Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita
Habari Mchanganyiko

Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kuhakikisha fedha zinazotolewa na kampuni hiyo kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii (CSR) zinagusa na kubadilisha maisha ya wananchi wa mkoa wa Geita na Tanzania kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mbali na kuipongeza GGML kwa kuja na teknolojia mbalimbali za uokoaji katika maonesho ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) yaliyofanyika kwenye viwanja vya General jijini Arusha, pia alieleza kuridhishwa na elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu masuala ya afya na usalama mahali pa kazi.

Makonda ambaye alitembelea banda la GGML katika maonesho hayo jana alisema mara nyingi maisha ya watu wa Geita hayafanani na utajiri uliopo katika mkoa huo.

“Mimi sioni aibu kuitwa tajiri,kwa sababu hilo ni jambo la kujivunia hivyo siwezi kujivunia umaskini ndio maana nataka ninyi Watanzania mliopo kwenye mgodi huu kuendelea kuwa chanzo cha mabadiliko ya watanzania wenzenu wanaozunguka mgodi huu,” alisema.

Aidha, Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk Kiva Mvungi alimpatia maelezo Makonda kwamba mpango wa CSR wa mwaka huu ni mwendelezo wa mipango ya awali unaolenga kujumuisha maendeleo yaliyofikiwa na GGML hadi sasa katika maeneo ya mazingira, miundombinu, afya, elimu na biashara ndogondogo na za kati (SMEs) katika jamii ya mwenyeji wa Geita.

Dk. Kiva alitoa mfano kuwa mwaka jana GGML imesaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) na wenyeji wake Halmashauri ya Mji Geita, Wilaya ya Geita pamoja na Halmashauri za jirani za wilaya za Chato, Bukombe na Mbogwe kutekeleza Mpango wa Uwajibikaji wake kwa Jamii (CSR) kwa mwaka 2022/2023 wenye thamani ya Sh bilioni 19.

“Jumla ya Sh bilioni 9.8 zilitengwa kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Geita ambapo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, bajeti ya Sh bilioni 8.6 ilitengwa.

“Uwepo wa GGML katika mkoa wa Geita umeonyesha matokeo chanya katika sekta ya elimu baada ya kampuni hiyo  kujenga miundombinu zaidi ya 1800 ya shule za msingi na sekondari katika wilaya ya Geita yenye halmashauri mbili za Geita mji na ile ya wilaya ya Geita,” alisema.

Alisema miundombinu hiyo imetokana na utekelezaji wa mabadiliko ya sheria ya madini ya mwaka 2017 ambapo GGML imekuwa ikiandaa mpango wa huduma kwa jamii kwa kushirikiana na halmashauri husika huku kila mwaka hutenga kiasi cha Sh 9.2 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Mbali na miradi ya elimu, Dk. Kiva alisema GGML kupitia fedha za CSR walitenga fedha kwa ajili ya miradi ya mazingira ambapo kiasi cha Sh700 milioni zinatumika.

“Ipo pia miradi ya kimkakati ukiwemo ule wa ufugaji wa samaki, miradi kwa kinamama na vijana pamoja na wasiojiweza ambapo zaidi ya Sh1.5 bilioni zinatumika.

Alisema miradi hiyo inaongeza thamani katika sekta mbalimba za kiuchumi na kuwapatia wananchi maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!