MAHAKAMA nchini Uganda imemfungulia rasmi mashtaka ya ufisadi na rushwa Waziri Marie Goretti Kitutu kutokana na tuhuma za kuuza mabati 14,500 ya kuezekea nyumba yaliyokusudiwa kuwasaidia raia wa huko Karamoja. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Licha ya Waziri Kitutu kukana mashtaka hayo, alirejeshwa rumande na kesi yake itasikilizwa tena ifikapo tarehe 12 Aprili mwaka huu.
Akihojiwa na Kamati ya Bunge mwezi uliopita, Marie Goretti Gitutu aliomba msamaha kwa usimamizi mbaya wa usambazaji wa mabati hayo.
Mawaziri kushtakiwa kwa ufisadi ni jambo la nadra nchini Uganda, ambako ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma ni jambo lililozoeleka.
Karamoja ni eneo la Uganda linalopakana na mataifa ya Kenya na Sudan Kusini, na wakazi wake ni wafugaji wanaohamahama ambao wako katika hatari ya kukumbwa na ukame na wizi wa mifugo.
Leave a comment