Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Watu milioni 7.3 kuamua hatima ya Senegal leo
Kimataifa

Watu milioni 7.3 kuamua hatima ya Senegal leo

Spread the love

RAIA milioni 7.3 wa Senegal leo Jumapili wanatarajiwa kupiga kura kuamua kati ya wagombea 17 ambao wanapepetana katika kinyang’anyiro cha kumrithi Macky Sall, ambaye ameongoza nchi hiyo tangu mwaka 2012.  Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).

Hapo awali uchaguzi huo wa urais uliopangwa tarehe 25 Februari mwaka huu lakini uliahirishwa kufuatia mzozo mkubwa wa kisiasa.

Senegal, nchi yenye wakazi milioni 18 lakini watu milioni 7.3 wanatarajiwa kushiriki katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo wa urais wa mwaka 2024 leo kati ya saa 8 asubuhi na saa 12 jioni.

Kura hiyo itamchagua rais wa tano wa Senegal, baada ya Léopold Sédar Senghor (1960-1980), Abdou Diouf (1981-2000), Abdoulaye Wade (2000-2012) na Macky Sall (2012-2024).

Wagombea 17 ambao wanashiriki kinyang’anyiro hiki cha urais kumrithi Macky Sall ni pamoja na Amadou Ba, Boubacar Camara, Aliou Mamadou Dia, Mamadou Lamine Diallo, El Hadji Mamadou Diao, Mahammed Boun Abdallah Dionne, Déthié Fall, Papa Djibril Fall, Bassirou Diomaye Faye, El Hadji Malick Gakou, Serigne Mboup, Daouda Ndiaye, Aly Ngouille Ndiaye, Anta Babacar Ngom, Khalifa Sall, Thierno Alassane Sall, Idrissa Seck.

Jumla ya vituo 16,440 vya kupigia kura vinafunguliwa leo pamoja na 807 nje ya nchi. Matokeo ya muda ya duru hii ya kwanza yatatangazwa kabla ya Ijumaa tarehe 29 Machi 224. Katika tukio la duru ya pili, hii itaandaliwa Jumapili ya pili baada ya Baraza la Katiba kutangaza matokeo ya mwisho ya duru ya kwanza.

Muhula wa Macky Sall unamalizika tarehe 2 Aprili mwaka huu. Tarehe 3 Februari  mwaka huu, mkuu huyo wa nchi anayemaliza muda wake alitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi huu uliopangwa kufanyika tarehe 25 Februari 2024.

Bunge lilipanga kufanyika uchaguzi tarehe 15 Desemba mwaka huu. Tarehe iliyokataliwa na Baraza la Katiba. Mwishoni mwa mdahalo wa kitaifa uliosusiwa na wagombea urais wengi, ulipanga ufanyike tareje 2 Juni 2024 tarehe ambayo pia ilifutiliwa mbali na Baraza la Katiba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!