Sunday , 12 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi
Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Waziri wa Madini, Doto Biteko
Spread the love

 

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameagiza waajiri kuhakikisha hakuna kifo chochote cha mfanyakazi kinachotokea mahali pa kazi kwani kila mtu ana thamani ya asilimia 100 kwa kila mtegemezi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Pia ametoa wito kwa kila mtu kuthamini maisha yake ili anapoenda kazini akiwa salama pia arejee akiwa salama bila madhara yoyote.

Biteko ametoa maagizo hayo leo Jumapili katika kilele cha maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayoendelea kwenye viwanja vya General Tyre jijini Arusha.

Biteko ambaye pia alitembelea mabanda ya maonesho ya taasisi na kampuni mbalimbali zilizopo kwenye maonesho hayo, amezipongeza kwa elimu kubwa ya afya na usalama wanayoendelea kuitoa.

“Japo tumejifunza bado zipo kazi za kufanya kwa sababu kuna mahali wamesema wana vifo vinne vilivyotokea mahali pa kazi. Wanakupa na asilimia utaona sifuri 0.01 lakini namba itakufanya uone ni la jambo kawaida lakini aliyefariki kwa mkewe, watoto, baba mkwe na majirani ni asilimia 100 na ndugu.

“Kifo cha mtu mmoja hasa kilichotokea mahali pa kazi hauwezi kukipima kwa tarakimu, kufanya hivyo ni kukidogosha. Kifo cha mtu mmoja ni kikubwa kinatakiwa kisitokee,” amesema Dk. Biteko.

Pia ametoa wito kwa waajiri wote wakati wote kuhakikisha wanarekodi ziro ya matukio ya vifo mahali pa kazi.

“Kwa waajiriwa napenda kuwasisitiza kwamba mtu wa kwanza kulinda usalama ni wewe muajiriwa mwenyewe, ukiona mtambo unaopaswa kuundesha na una kasoro na umelazimishwa na muajiri kuuendesha, unapaswa uwe wa kwanza kusema mtambo huu haupo salama na usihesabike kuwa mtu uliyegoma kwa sababu pia una wajibu kulinda usalama wako,” amesema.

Aidha, alitoa wito kwa Wakala wa Afya na Usalama mahali pa kazi (OSHA) kuendelea kutoa elimu ya afya na usalama kila mahali.

Pia aliwataka OSHA kuendelea kubadilika kwa kuondokana na utaratibu wa zamani wa kuwa kama afisa wa polisi pindi anapofika kwenye ofisi ya muajiri kila mmoja anatetemeka.
“Inatakiwa ofisa wa OSHA akija watu wafurahi. Tusitumie faini kama ndilo jukumu la kwanza kwamba ndio kitu pekee cha kufuata kwa wamiliki wa viwanda.

“Osha alikuwa bize na faini pia hakuwa na mahusiano mazuri na taasisi nyingine lakini sasa ni lazima tujenge uhusiano ili kazi yetu isiwe ya kipolisi… mambo ya ksuema haunijui mimi ni nani yaishe! Shughulika na kazi yako.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama mahali pa kazi (OSHA), Hadija Mwenda alisisitiza kuwa wataendelea kusimamia majukumu yao ipasavyo kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa.

“Tutaendelea kuhamasisha kuwezesha maeneo ya kazi yawe salama. Suala la usalama na afya ni suala la kujenga tabia na ujengaji tabia ni jambo linatokana na kuelimishwa,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!