Sunday , 12 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji
Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love

 

BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua hatua stahiki katika kuhakikisha inatekeleza agizo la Makamu wa Rais, Dk. Philipo Isory Mpango kwa kupanda miti 2,000,000 kwa kila mkoa ikiwa ni mkakati wa uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji katika bwawa la Mindu. Anaripoti Yusuph Kayanda, Morogoro … (endelea).

Akikagua eneo la mradi wa uhifadhi wa mazingira katika bwawa la Mindu, lililopo Manispaa ya Morogoro linalosimamiwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Godfrey Eliakumu Mnzava amepongeza hatua madhubuti zinazochukiwa na bonde hilo katika kutunza vyanzo vya maji kwa kuendelea kuhamasisha zoezi la upandaji wa miti ambapo mpaka sasa takribani miti elfu 24,255 imekwisha pandwa katika mradi huo.

“Hata kwa kuangalia inaonesha watu wapo serious (makini) kwenye upandaji wa miti katika chanzo hiki cha maji, Lakini pia tumepata wasaa wa kuona miti iliyopandwa katika Mwenge wa Uhuru 2023 na namna ambavyo inaendelea, Mlipanda miti 2,000 na miti 1,939 inaendelea vizuri, Wenzetu wa Wami wanaendelea kurudishia miti 61 ambayo imekufa, Hii kazi mmeifanya vizuri kwenye eneo la utunzani wa mazingira na upandaji miti, Wenzetu wa Wami Ruvu hatuwadai chochote.” alisema Mnzava.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Rebeca Nsemwa alitumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi wa Manispaa ya Morogoro na Kikosi cha Jeshi la Mzinga kwa kuungana na serikali katika ulinzi na utunzaji wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya vyanzo vya maji, ambapo mpaka sasa miti miti 76,926 ikipandwa katika maeneo ya shule, hifadhi ya milima Uruguru, bwawa la Mindu pamoja na eneo la Jeshi Magadu.

Mradi wa uhifadhi wa mazingira katika bwawa la Mindu umegharimu zaidi ya Sh.50 milioni ambazo ni michango ya miche na nguvu kazi ya jamii ikiwa na lengo la kulinda chanzo hiko cha maji kinachotegemewa na kwa zaidi ya 70% na wakazi wa Manispaa ya Morogoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!