Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Silaa atoa maagizo 3 matumizi ya ardhi
Habari za Siasa

Silaa atoa maagizo 3 matumizi ya ardhi

Jerry Silaa
Spread the love

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amepiga marufuku kubadili matumizi ya eneo kwa kutumia mabango ya vitambaa na badala yake ni lazima uitwe mkutano wa wananchi wa mtaa mzima watu warekodi kwa simu zao ili kuweka ushahidi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Silaa amesema hayo leo Jumapili wakati alipofanya ziara katika maeneo ya Oysterbay na Msasani jijini Dar es salaam akiongozana na viongozi wakuu wa Wizara yake  na kukuta ambapo baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wameanza kujenga vyumba vya biashara ya kupangisha kinyume na matumizi ya maeneo hayo ambayo ni makazi.

Akitoa maelekezo, Silaa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake kuunda Kamati Maalumu itakayopitia kiwanja kwa kiwanja ili kubaini viwanja vilivyobadilishwa matumizi na kuvifanyia marekebisho pamoja na kuwaelimisha wananchi wa mitaa hiyo namna bora ya kubadili matumizi.

Maelekezo ya tatu ya Waziri Silaa ni kwa Watanzania wote ambao wanataka kubadili maeneo yao ya makazi kuwa ya biashara basi wawe waungwana kwa kuweka nafasi ya kutosha kwa ajili ya wateja, wapita njia na wananchi wa mtaa huo kupita bila kubabaika.

Waziri Silaa amesisitiza kuwa maeneo ya Oysterbay, Masaki na Msasani ni maeneo nyeti ya makazi yanayobeba taswira njema kwa wawekezaji na wageni kutoka nje, hivyo si vyema kuyafanya yenye vibanda vya biashara badala ya makazi.

Xxxxx

Watu milioni 7.3 kuamua hatima ya Senegal leo

RAIA milioni 7.3 wa Senegal leo Jumapili wanatarajiwa kupiga kura kuamua kati ya wagombea 17 ambao wanapepetana katika kinyang’anyiro cha kumrithi Macky Sall, ambaye ameongoza nchi hiyo tangu mwaka 2012.  Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).

Hapo awali uchaguzi huo wa urais uliopangwa tarehe 25 Februari mwaka huu lakini uliahirishwa kufuatia mzozo mkubwa wa kisiasa.

Senegal, nchi yenye wakazi milioni 18 lakini watu milioni 7.3 wanatarajiwa kushiriki katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo wa urais wa mwaka 2024 leo kati ya saa 8 asubuhi na saa 12 jioni.

Kura hiyo itamchagua rais wa tano wa Senegal, baada ya Léopold Sédar Senghor (1960-1980), Abdou Diouf (1981-2000), Abdoulaye Wade (2000-2012) na Macky Sall (2012-2024).

Wagombea 17 ambao wanashiriki kinyang’anyiro hiki cha urais kumrithi Macky Sall ni pamoja na Amadou Ba, Boubacar Camara, Aliou Mamadou Dia, Mamadou Lamine Diallo, El Hadji Mamadou Diao, Mahammed Boun Abdallah Dionne, Déthié Fall, Papa Djibril Fall, Bassirou Diomaye Faye, El Hadji Malick Gakou, Serigne Mboup, Daouda Ndiaye, Aly Ngouille Ndiaye, Anta Babacar Ngom, Khalifa Sall, Thierno Alassane Sall, Idrissa Seck.

Jumla ya vituo 16,440 vya kupigia kura vinafunguliwa leo pamoja na 807 nje ya nchi. Matokeo ya muda ya duru hii ya kwanza yatatangazwa kabla ya Ijumaa tarehe 29 Machi 224. Katika tukio la duru ya pili, hii itaandaliwa Jumapili ya pili baada ya Baraza la Katiba kutangaza matokeo ya mwisho ya duru ya kwanza.

Muhula wa Macky Sall unamalizika tarehe 2 Aprili mwaka huu. Tarehe 3 Februari  mwaka huu, mkuu huyo wa nchi anayemaliza muda wake alitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi huu uliopangwa kufanyika tarehe 25 Februari 2024.

Bunge lilipanga kufanyika uchaguzi tarehe 15 Desemba mwaka huu. Tarehe iliyokataliwa na Baraza la Katiba. Mwishoni mwa mdahalo wa kitaifa uliosusiwa na wagombea urais wengi, ulipanga ufanyike tareje 2 Juni 2024 tarehe ambayo pia ilifutiliwa mbali na Baraza la Katiba.

1 Comment

  • Silaa, huku viwege kwa mpemba mtaa wa magari, Kuna kanisa linaitwa emous bible church wamelijenga ndani ya mkondo wa maji. Wananchi tunateseka maji yanabomia nyumba za watu hayana pa kwenda. Tunaomba msaada wako. Serikali ya mtaa , wajumbe wa mtaa mpaka diwani wanazo taarifa. Wakija wanahobgwa hela wanaondoka. Kaka njoo utupatie utatuzi. Kwa mjumbe winni, na baba koku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!