Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Samsung yazindua muonekano wa vifaa kwa 3D kwa kutumia SmartThings na AI 
Biashara

Samsung yazindua muonekano wa vifaa kwa 3D kwa kutumia SmartThings na AI 

Spread the love

 

KAMPUNI ya Samsung Electronics Co. Ltd imezindua huduma ya itakayomwezesha mteja kupata muonekano wa ramani kwa 3D, huduma hii imezinduliwa kwa mara ya kwanza katika kongamano kubwa la teknolojia na ubunifu duniani (CES) 2024 na sasa inapatikana katika nchi zote zinazoweza kupata huduma ya SmartThings. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Huduma hii inayojulikana kama ‘Map View’ huboresha usimamizi wa shughuli za nyumbani kwa kubadilisha mpangilio wa vifaa vyako kuwa picha halisi kupitia programu ya SmartThings. Watumiaji wanaweza kuona vifaa vyao kwa uhalisia na kurekebisha mwanga, halijoto, ubora wa hewa na matumizi ya nishati kwa urahisi muda wowote na mahali popote.

‘Map View’ inatoa ufumbuzi wa changamoto ya kudhibiti idadi inayoongezeka ya vifaa vilivyounganishwa katika majumbani duniani kote na hurahisisha ufanisi wa usimamizi ili kuondoa hitaji la kusimamia kila kifaa pekee yake unapotaka kukitumia. Huduma hii inawonyesha watumiaji mwonekano mzima wa nyumba yao kwa wakati mmoja na inawapatia taarifa kwa wakati halisi kadiri vifaa vingine vinavyoendelea kuunganishwa.

Toleo lililopita la ‘Map View’ lilikuwa la muundo wa 2D ambao ulifanya kazi kwa nyumba ambazo zilikuwa na ramani pekee. Hivyo, toleo hili jipya lililoboreshwa la 3D limekuja na fursa ya huduma za ‘Spatial AI’ katika vifaa vya Samsung – kama vile ‘Bespoke Jet Bot™’ – inayotumia sensa za ‘LiDAR’ kwenye kifaa kupima kwa uhakika na kuonyesha mwonekano sahihi wa mpangilio wa nyumba. Sasa, watumiaji wanaweza kuelewa kwa urahisi zaidi muundo na hali ya nafasi ya nyumba zao kwa mwonekano wa 3D.

Huduma hii pia imeimarisha utendaji kazi wake wa kifaa chake cha kuainisha vitu ili kuruhusu ufuatiliaji na udhibiti bora wa vifaa vinavyohitajika. Inalenga kutoa huduma mahiri mahususi kwa kila mtumiaji na rafiki kwa kutumia uwezo wa AI, ambayo pia ilizinduliwa katika kongamano la CES 2024, kufikia mwisho wa mwaka.

Upatikanaji

‘Map View’ inapatikana kupitia applikesheni ya SmartThings kwenye vifaa vya mkononi vya Android na iOS, pamoja na luninga. Udhibiti wa huduma hii pia utapatikana kupitia njia zingeine za ziada, kama vile majokofu ya ‘Family Hub™’, ndani ya nusu ya kwanza ya mwaka.

Hapo awali, ‘Map View’ ilizinduliwa nchini Korea na Marekani mwaka jana. Lakini sasa, inaweza kutumika katika nchi zote zilizofikiwa na huduma ya SmartThings.

“Samsung inafanya kazi kwa bidii kuwawezesha wateja kusimamia vifaa vyao vya nyumbani bila usumbufu muda wowote na mahali popote, na ‘Map View’ ni matokeo ya juhudi hizi” alisema Seungbeom Choi, Mkuu wa Kituo cha Mfumo wa Vifaa wa Samsung Electronics. “Tutaendelea kutambulisha huduma na vifaa mbalimbali vinavyohitajika ili wateja wetu waweze kufurahia matumizi na maisha bora nyumbani kwao.”

Samsung kwa sasa inashirikiana na makampuni ya ujenzi kupanua zaidi huduma ya ‘Map View’ kuzifikia sio nyumba tu pekee bali nyumba za biashara na maofisini. Kampuni inalenga kusaidia kutengeneza mazingira ya kisasa kwa wateja duniani kote kwa kuongeza utendaji wake. Hii inajumuisha matumizi bora ka mtumiaji (UX) kwa ‘skrini’ kubwa ambayo itamsaidia watumiaji wa biashara kwa biashara (B2B) kwa kutumia alama, na huduma ya ‘Quick Control’, ambayo huwawezesha watumiaji kufikia huduma muhimu kwa urahisi.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

error: Content is protected !!