WATU takribani 100 wamefariki dunia nchini Syria, kutokana shambulio la ndege zisizo na rubani liliopiga kwenye Chuo cha kijeshi cha taifa hilo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Ndege hizo zisizo na rubani zinadaiwa kubeba vilipuzi ambavyo viliathiri mamia ya watu waliokuwepo katika chuo hicho kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuhitimu mafunzo. Miongoni mwa waliopoteza maisha ni wanawake na watoto.
Waziri wa Afya Syria, Hassan al-Gabbash, amesema watu zaidi ya 200 wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Jeshi la Syria limelaumu vikundi vya kigaidi likidai vimetekeleza tukio hilo la mauaji ya mamia ya watu wasiokuwa na hatia.
Leave a comment