Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa apiga marufuku watumishi kujitolea ardhi
Habari za Siasa

Majaliwa apiga marufuku watumishi kujitolea ardhi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amepiga marufuku watumishi wa kujitolea katika sekta ya ardhi, hususan kwenye eneo la upimaji viwanja, akisema wanachochea migogoro kutokana na wengi wao kutokuwa waaminifu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Waziri Majaliwa ametoa marufuku hiyo leo tarehe 6 Oktoba 2023,jijini Dodoma, akizungumza na viongozi wa majiji ya Arusha, Mwanza, Dar es Salaam,Mbeya na Tanga, kuhusu migogoro ya ardhi iliyoko katika maeneo yao.

“Afisa mipango miji, majiji , halmshauri na manispaa hawana sababu ya kuchukua watu wa muda kufanya kazi ya upimaji, wafanye wao. Kama ni lazima wafanye shughuli nyingine sababu ukiwakabidhi eneo hilo la kuwasiliana na wateja lazima wafanye tofauti kwanza hawana mishahara wanajitolea,” amesema Waziri Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Majaliwa, ameagiza kampuni za upimaji ardhi jijini Dodoma zilizoshindwa kutekeleza majukumu yake, zichukuliwe hatua za kisheria “moja kati ya hatua hizo tuzi- blacklist, kwa sababu makampuni yako mengi yapo waaminifu.”

Kiongozi huyo amesema, kampuni hizo zimekuwa zikichochea migogoro, huku akidai nyingi zinamilikiwa na viongozi wa jiji hilo.

Aidha, Waziri Majaliwa,ameagiza watumishi wanne wa kujitolea katika sekta ya ardhi jijini Dodoma, akiwemo Justine Albert na Fred Mathias , wachunguzwe kwa tuhuma za kutumia nyaraka za serikali kwa kushirikiana na viongozi, kuuza viwanja kiholela.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!