Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watoto 900 kunufaika na mradi LFTW
Habari Mchanganyiko

Watoto 900 kunufaika na mradi LFTW

Spread the love

SHIRIKA la Light for the World Tanzania wametoa pikipiki 20 za  kuwawezesha walimu wa elimu maalumu na vifaa mbalimbali vya kufundishia kwa watoto wenye uoni hafifu vyote vikiwa na thamani ya Sh 65 milioni ambavyo vinatarajiwa kunufaisha zaidi  ya watoto 900 katika mradi huo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 26 Julai 2023 na Mkurugenzi mkazi wa shirika hilo, Joseph Banza katika kikao cha kwanza cha utekelezaji rasmi mradi wa elimu jumuishi na ufundishaji tembezi kwa watoto wenye changamoto ya macho katika mikoa ya Dodoma na Morogoro.

Mmoja wa walimu tembezi akikabidhiwa kadi ya pikipiki na mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Elimu Maalumu TAMISEMI, George Mbijima.

Banzai amesema shirika hilo kwa kushirikiana na TAMISEMI, wakuu wa mikoa ya Dodoma na Morogoro, idara ya elimu ya msingi na sekondari imeandaa kikao kazi cha watendaji wa elimu maalumu katika ngazi ya mikoa na halmashauri katika mikoa ya utekelezaji wa mradi huo hususani wenye changamoto ya uoni katika mikoa ya Dodoma na Morogoro.

Amesema lengo kuu ni kukazia uelewa, kupanga mipango na kutoa fursa ya majadiliano yahusuyo mradi wa elimu jumuishi na elimu maalum kwa watoto hao unaoendeshwa katika halmashauri 14 ndani ya mikoa ya Dodoma na Morogoro.

Aidha, amesema kuwa malengo mahususi ya kikao hicho ni kuutambulisha mradi mkubwa wa miaka mitano unaofadhiliwa na shirika hilo “Inclusive Vision 2022-2026” ambao unatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Ruvuma kwa washiriki wa kikao kazi.

Katika utekelezaji wa mradi huo pia amesema malengo mengine ni kutoa maelezo ya kina juu ya wa elimu jumuishi na elimu maalumu kwa watoto wenye mahitaji maalumu na kutoa fursa kwa washiriki kuuliza maswali na kupata ufafanuzi juu ya mradi huo.

Amesema kuwa mradi umekabidhi pikipiki 20 za kuwawezesha waalimu wa elimu maalumu ili waweze kutimiza majukumu yao kama waalimu tembezi kwa ubora na ufanisi.

“Jumla ya pikipiki 20 zimegawiwa katika mgawanyo wa mikoa ambapo pikipiki 12 zimetolewa kwa walimu wa Morogoro na 8 kwa walimu wa Dodoma na jumla ya gharama hizo ni milioni 49.

“Pia pikipiki hizo zina bima kubwa,pamoja na vifaa mbalimbali kufundishia watoto wenye changamoto ya uoni hafifu na mahitaji maalumu vyenye thamani ya sh.mil.16 na kufanya gharama yote kuwa sh.mil.65,” ameeleza Banza.

Hata hivyo Banza ameeleza kuwa hadi mradi huo unaisha utawanufaisha watoto hususani wenye mahitaji maalumu 900.

Kwa upande wa mgeni rasmi ambaye amefungua kikao hicho Naibu Mkurugenzi Elimu Maalumu Tamisemi, George Mbijima amewataka watendaji kuhakikisha wanawapatia elimu watoto wenye mahitaji maalumu kama mwongozo wa elimu unavyotaka.

Mbali na hilo amesema vifaa vilivyotolewa na shirika hilo vinatakiwa kutumiwa kwa mujibu wa malengo na kuhakikisha elimu inakuwa shirikishi jambo ambalo litasaidia serikali kutekeleza malengo yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafugaji kuku Ihemi wanufaika na mafunzo

Spread the loveWADAU  wa mnyororo wa thamani katika sekta ndogo ya kuku...

error: Content is protected !!