Saturday , 11 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu agomea wito wa DCI
Habari za SiasaTangulizi

Lissu agomea wito wa DCI

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Tundu Lissu, amegoma kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), kwa ajili ya uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili, akidai barua ya wito huo haijabainisha kosa analotuhumiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Lissu ametoa msimamo huo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam,  baada ya kuwasili nchini akitokea nje ya nchi kwa mapumziko mafupi. Ikiwa ni siku nane tangu ofisi ya DCI imwandikie barua ya wito.

Alipoulizwa kama atafika ofisini kwa DCI, Lissu alijibu “kufanya nini? Unapoitwa na Polisi mahali kokote lazima Polisi akuambie anakuita kwa kosa gani, ile barua imesema kuna kosa?”

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyoandikwa na ACP Joseph Mfungomara, kwa niaba ya DCI Ramadhan Kingai, Lissu ametakiwa kufika Polisi kwa ajili ya kusaidia uchunguzi unaofanywa kuhusiana na maneno yanayodaiwa kutokuwa na staha aliyotoa dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Ili tuweze kukamilisha uchunguzi wetu, ofisi hii inakutaka ufike ofisi ya DCI makao makuu ndogo Dar es Salaam, siku ya Alhamisi, tarehe 20 Julai 2023, saa 3.00 kamili asubuhi bila kukosa kwa ajili ya mahojiano,” imesema barua hiyo.

Lissu anadaiwa kutoa lugha isiyo na staha dhidi ya Rais Samia, wakati akizungumzia mjadala wa sakata la bandari nchini, ambapo mwanasiasa huyo alipinga mkataba wa ushirikiano wa kiserikali kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai, kwa madai kuwa hauna maslahi kwa taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!