Saturday , 30 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Watoto 500 wafariki kwa njaa
Kimataifa

Watoto 500 wafariki kwa njaa

Spread the love

SHIRIKA la kimataifa la hisani la Save the Children limesema takriban watoto 500 wamefariki kutokana na njaa nchini Sudan. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Shirika hilo kati ya watoto hao 500 pia wapo watoto zaidi ya 20 katika kituo cha watoto yatima kinachosimamiwa na serikali katika mji mkuu Khartoum, tangu mapigano yalipozuka nchini humo mwezi Aprili mwaka huu.

Shirika la Save the Children pia lilisema kuwa karibu watoto 31,000 wanakosa huduma ya lishe na matibabu ya utapiamlo tangu shirika hilo la misaada kusitisha shughuli zake kwenye vituo 57 vya lishe nchini Sudan.

Mzozo huo wa Sudan umegeuza jiji la Khartoum na maeneo mengine ya mijini kuwa viwanja vya vita. Wakazi wengi wanaishi bila maji na umeme, na mfumo wa huduma za afya nchini humo umeporomoka.

Mkurugenzi wa shirika la Save the Children nchini Sudan, Arif Noor amesema hawakutegemea kuwaona idadi kubwa ya watoto kama hao wakifa kwa njaa.

Noor amesema mbali na watoto hao kufa njaa idadi ya watoto walioachishwa shule nchini humo pia imeongeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!