Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania, Cuba kuwanoa wanasiasa vijana
Habari za Siasa

Tanzania, Cuba kuwanoa wanasiasa vijana

Spread the love

Tanzania na Cuba zimekubaliana kushirikiana na kuimarisha misingi ya kisiasa, ujengaji wa uwezo kwa wanasiasa vijana, sekta za elimu, afya, utalii, biashara na uwekezaji. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hayo yamebainishwa leo Jumatano na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipokutana na kuzungumza na Balozi wa Cuba nchini, Yordenis Despaigne Vera katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

“Tanzania imekuwa ikishirikiana na Cuba kwa muda mrefu na ushirikiano baina ya mataifa haya umekuwa imara tangu ulipooasisiwa na viongozi wakuu wa Mataifa hayo Hayati Fidel Castro na Hayati Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,” amesema Balozi Mbarouk.

Balozi Mbarouk ameongeza kuwa kwa sasa Cuba imeonesha dhamira ya kushirikiana Tanzania katika kuimarisha misingi ya siasa, kuwajengea uwezo wanasiasa vijana pamoja na sekta nyingine kama vile elimu, afya, na utalii pamoja na kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya biashara na uwekezaji

Kwa upande wake Balozi wa Cuba nchini, Yordenis Despaigne Vera amesema kwamba Cuba inajivunia kuwa na uhusiano imara na Tanzania kwa takribani miaka 60.

Amesema Cuba itaendelea kushirikiana na Tanzania kuimarisha misingi ya kisiasa kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

“Wakati umefika sasa kwa serikali zetu mbili (Cuba na Tanzania) kuimarisha ushirikiano wake kisiasa na kuhakikisha kuwa mataifa yetu yanakuwa na misingi imara ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi pia kwa manufaa ya pande zote mbili,” amesema Balozi Vera.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!