Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wateja wa M-Pesa sasa kupokea pesa kutoka nchi 21 za Ulaya
Habari Mchanganyiko

Wateja wa M-Pesa sasa kupokea pesa kutoka nchi 21 za Ulaya

Afisa Mtendaji Mkuu na Mwanzilishi mwenza wa NALA, Benjamin Fernandes akionyesha jinsi ya Nala inavyofanya kazi
Spread the love

 

WATEJA wanaotumia mtandao wa simu wa Vodacom kupitia M-Pesa sasa wanaweza kupokea fedha kutoka katika nchi za Marekani, Uingereza, Ujerumani na nchi 19 zilizokuwepo katika Umoja wa Ulaya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Kampuni ya Vodacom Tanzania kusaini mkataba na Kampuni ya NALA ya Tanzania, inayoshughulika na mfumo wa malipo duniani kote ambapo itawawezesha Watanzania waishio katika nchi hizio kutuma pesa nchini kupitia mfumo wa M-Pesa.

Kampuni ya NALA, ambayo imeanzishwa nchini Tanzania ni taasisi ya huduma za kifedha kidijitali (Fintech company), ilianza huduma zake nchini Uingereza na baadaye Marekani na sasa imetimiza lengo lake la kuiunganisha Dunia kuwawezesha Waafrika kwa kuongeza nchi 19 zilizopo katika umoja wa Ulaya.

Ukiacha nchi za Marekani na Uingereza nchi nyingine ambazo zinaweza kutuma fedha kwa M-Pesa ni pamoja na nchi za Austria, Ubelgiji, Cyprus, Estonia, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ugiriki, Ireland, Italia, Lithuania, Luxembourg, Malta, Uholanzi, Ureno, Slovakia, Slovenia na Hispania.

Afisa Mtendaji Mkuu na Mwanzilishi mwenza wa NALA, Benjamin Fernandes alisema, akiwa ni Mtanzania, inampa furaha kuwafikia robo ya Waafrica wanaoishi Ulaya kwa kuwapa huduma rahisi na ya kuaminika ya kutuma pesa nyumbani.

“Kupitia Vodacom M-Pesa tunaiunganisha miundombinu na hivyo kuleta daraja la malipo kati ya nchi za Uingereza, Marekani na jumuiya ya Ulaya na Tanzania.

“NALA imekuwa kwa haraka zaidi na kuongeza wigo wake kijiografia, kupitia bidhaa na pia kwa kuboresha miundombinu yetu. Ushirikiano tuliozindua leo na M-Pesa ya Vodacom utatuwezesha kuongeza wigo wa kutuma na kupokea pesa kutoka nchi nyingi zaidi duniani, kwa pamoja tunaendeleza nia yetu ya kuleta fursa za kiuchumi kwa waafrika pote duniani,” amesema Fernandes.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa M-Commerece, Epimack Mbeteni, aliupongeza ushirikiano huo huku akiongeza kwamba unaendana na mipango ya kampuni katika kukuza huduma ya utumaji pesa kimataifa (IMT).

Mkurugenzi wa M-Commerece, Epimack Mbeteni akizungumza

Amesema wateja wa Vodacom M-Pesa sasa wanaweza kutuma na kupokea pesa kutoka nchi zaidi ya 200 moja kwa moja kwenda kwenye akaunti zao za M-Pesa.

“Tumetumia ubunifu na ushirikiano wetu ili kuhakikisha tunawezesha utumaji na upokeaji pesa kimataifa katika bara la Afrika na dunia kwa ujumla na hivyo kuiwezesha dunia kutuma pesa kirahisi zaidi na hivyo kuwezesha biashara kati ya mipaka ya nchi.

“Tunaendelea kuongeza faili letu kwa kupitia ushirikiano na makampuni mbalimbali, tunafuraha kushirikiana na NALA kampuni ambayo inatokea hapa hapa nchinilakini inabadilisha namna na jinsi ya kutuma pesa duniani,” amesema Mbeteni.

Ushirikiano huu utaambatana na kampeni itakayowazawadia wateja wa NALA na M-Pesa pindi watakapotumia huduma hii. NALA itawazawadia wateja wapya kiasi cha dola 10 pindi watakapotuma kwa mara ya kwanza, lakini pia kutakuwa na nafasi ya kujishindia tiketi mbili za ndege (kwenda na kurudi) kwa wateja watakaotuma pesa kwenda M-Pesa, kwa wateja watakaotuma au kupokea pesa katika kipindi cha mwezi Aprili kwa ajili ya Pasaka au Eid.

Kwa nchi za Jumuiya ya Ulaya, NALA inapatikana kwenye App Store na Play Store kwa ajili ya kupakua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

error: Content is protected !!