Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Sheria ya kuwabana wenye nyumba yaja,Waziri Mabula ataka madalali wawe na maadili
Tangulizi

Sheria ya kuwabana wenye nyumba yaja,Waziri Mabula ataka madalali wawe na maadili

Spread the love

SERIKALI imesema inakamilisha Muswada wa Sheria utakaoanzisha chombo cha kusimamia sekta ya milki (Real estate Regulatory Authority), kwaajili ya kusimamia na kulinda maslahi ya wapangaji. Anaripoti Mwandishi Wetu….(endelea)

Pamoja na shughuli zingine chombo hicho kitamlazimisha mwenye nyumba kutoza kodi ya mwezi mmoja mmoja badala ya utaratibu wa sasa ambapo yeye huamua kupokea kodi ya kuanzia miezi sita hadi mwaka mmoja.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula, wakati akifungua mafunzo ya wiki moja kwa mawakala wa mali zisizohamishika.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Chuo cha Biashara (CBE) kwa wiki moja na bada ya muda yatakuwa yakifanyika kwa muda wa mwaka mmoja.

Waziri alisema kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu wenye nyumba kuwalazimisha kulipa kodi ya miezi sita au mwaka mmoja hivyo sheria hiyo itasaidia kusimamia maelekezo ya serikali.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara, Profesa Tandi Luoga akizungumza na viongozi wenzake wakati wakimsubiri Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula, wakati akifungua mafunzo ya wiki moja kwa mawakala wa mali zisizohamishika

Aliipongeza CBE kwa kuanzisha kozi hiyo aliyosema imekuja wakati mwafaka.

“Sheria hii italazimisha mwenye nyumba kupokea kodi ya mwezi mmoja mmoja lakini itaweka nafasi ya majadiliano baina ya mpangaji na mwenye nyumba na wakizungumza wakikubaliana kulipa mwaka au miezi sita kwa hiyari hiyo inaruhusiwa lakini haipaswi kuwa lazima,” alisema

Dk. Mabula aliwataka mawakala nao kuzingatia maadili ili kuifanya kazi hiyo kuwa na heshima kama ilivyo kwa nchi nyingi za Afrika Mashariki kwani uzoefu unaonyesha kwamba madalali wengi wamekuwa wakifanya kazi hiyo kiholela.

Alisema baadhi ya madalali wamekuwa na kawaida ya kupandisha gharama ya nyumba na vyumba vya kupangisha kwa lengo la kupata kamisheni kubwa hali ambayo inaumiza wananchi wengi hasa wenye uwezo mdogo.

“Unakuta nyumba inapangishwa kwa Sh 100,000 kwa mwezi lakini dalali anamwambia mpangaji kwamba inapangishwa kwa Sh 200,000 sasa mpangaji akijiongeza akaenda kwa mwenye nyumba akaambiwa kwamba inapangishwa kwa Sh 100,000 heshima yako na uaminfu wako unapotea,” alisema Dk. Mabula.

Alisema baadhi yao wamekuwa wakiuza mali ambazo hawajaambiwa kuuza kama viwanja na nyumba hali ambayo imesababisha migogoro mingi huku wao wakitoweka kusikojulikana na kusababisha wanunuzi kubaki wakihangaika.

“Ndiyo maana nasisitiza kwenye mafunzo haya muwafundishe maadili. Ukiwa na maadili watu watakuwa mabalozi wako kwamba ukitaka kazi hii ifanikiwe mwone fulani lakini kama ni tapeli hutapata kazi na utaishia kutafutwa kwa wizi,” alisema,” alisema Waziri Mabula.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula, akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo ya wiki moja kwa mawakala wa mali zisizohamishika katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)

Mwenyekiti wa Chama cha Madalali Tanzania (AREA), Erick Rweikiza alisema dhamira ya chama hicho ni kuweka mazingira bora ya kuelimisha wanachama wake kuhusu taaluma yao na kujenga umoja kibiashara na kutetea maslahi yao.

Alisema nia yao ni kuweka mazingira bora ya kutoa huduma bora kwa wapangaji, wapangishaji, wauzaji na wanunuzi ambao kwa pamoja ndio waajiri wa mawakala hao.

“Pamoja na madalali walengwa wetu wakubwa ni pamoja na watu wote wasio na ajira na nia yetu ni kuwafundisha watu wasio na ajira wajiajiri kupitia taaluma hiyo,” alisema Rweikiza

Aidha, alisema takwimu zinaonyesha kuwa Jiji la Dar es Salaaam litakuwa na watu milioni 10 ifikapo mwaka 2030 hivyo ongezeko hilo la idadi ya watu itasababisha mahitaji ya makazi kuwa makubwa hivyo kutoa fursa kwa madalali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!