Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko LSF yazindua mradi kuwezesha wanawakekiuchumi, 1,423 kunufaika Arusha
Habari Mchanganyiko

LSF yazindua mradi kuwezesha wanawakekiuchumi, 1,423 kunufaika Arusha

Spread the love

 

SHIRIKA la Legal Services Facility (LSF), limezindua mradi wa kuwawezesha kiuchumi wanawake jamii ya kimasai waishio wilayani Longido, Mkoa wa Arusha, ambapo unatarajiwa kuwanufaisha moja kwa moja watu 1,423. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Mradi huo wa miaka miwili (2023/24), umezinduliwa jana tarehe 30 Januari 2023 jijini Arusha, ambapo LSF imeshirikiana na Taasisi ya North-South Cooperation kutoka nchini Luxembourg.

Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala amesema kuwa LSF imeamua kutekeleza mradi huo kwa kushirikiana na wadau wengine, ili kusaidia jamii ya kimasai hususani wanawake na watoto wa kike, ambao wamekuwa nyuma katika hatua za maamuzi, umiliki wa rasilimali ikiwemo ardhi na mifugo, pamoja na fursa sawa ya kwenda shule.

“Jamii ya kimasai ni ya kipekee nchini Tanzania kutokana na udumishaji wa mila na desturi zake kwa kipindi kirefu. Uchumi wa jamii ya kimasai unategemea zaidi shughuli za ufugaji kwa asilimia 85 ya shughuli zote za kiuchumi zinazoendeshwa na jamii hii. Njia kuu za uchumi pamoja na uzalishaji mali kwa jamii ya kimasai zinamilikiwa na kuendeshwa na wanaume,” alisema Lulu na kuongeza:

“Hali inayosababisha haki za wanawake na wasichana wa kimasai kukiukwa. Kuanzishwa mradi huu hapa Longido utawezesha kutatua baadhi ya changamoto hizi na kuwawezesha wanawake wa kimasai kijamii na kiuchumi.”

Kwa upande wake Diwani wa Namanga, Hassan Ngoma ambaye amemuwakilisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido, ameipongeza LSF pamoja na wadau wa maendeleo kutoka Luxemburg kwa kuona vyema na kuamua kushirikiana kutekeleza mradi huu..

Amesema mpango wa mradi huo kufanya ujenzi wa mabweni ya watoto wa kike katika shule za sekondari za Lekule na Namanga, utawezesha kutatua changamoto ya wanafunzi kurundikana kwenye bweni, kuongeza idadi ya watoto shuleni na kuboresha mzingira ya utoaji wa elimu utakaochochea ufaulu wa wanafunzi kuongezeka.

“Natoa wito kwa jamii kutumia fursa kwa kushiriki kikamilifu na kutunza miundo mbinu itakayotolewa kupitia mradi huu. Tunawahakikishia serikali itaendelea kuboresha miundo mbinu katika ya shule ikiwemo upatikanaji wa umeme katika shule ya Lekule ili kwenda sambaba na uboreshwaji wa mazingira ya elimu katika wilaya yetu,” amesema Ngoma.

Akitoa neno la shukurani kwa njia ya mtandao wakati wa uzinduzi, Muwakilishi kutoka North-South Cooperation, Roberto Marta amesema, utekelezaji wa mradi wa ‘Wanawake Tunaweza’ umekuja mara baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya North-South Cooperation, LSF, wanufaika tarajiwa wilayani Longido, mamlaka za serikali ikiwemo wilaya na kata husika, pamoja na wasaidizi wa kisheria wilayani Longido.

“Mradi huu tutautekeleza kwa pamoja na LSF ikiwa ni sehemu ya ufadhili wa Serikali ya Luxembourg kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Ulaya (Luxembourg Ministry of Foreign and European Affairs) kwa kushirikiana na Idara ya Ushirikiano wa Maendeleo (Directorate of Development Cooperation). Mradi huu unawiana kabisa na mkakati wa ushirikiano wa kimaendeleo wa Luxembourg kuelekea 2030 unaotoa kipaumbele kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kama nguzo muhimu ya kupambana na umasikini na kufikia maendeleo endelevu,” amesema Roberto.

Mradi wa ‘Wanawake Tunaweza’ utatekelezwa kwa miaka miwili ili kuchochea maendeleo kijamii na kiuchumi kwa jamii ya kimasai hasa wanawake na watoto wa kike katika jamii hiyo kwa kuwezesha kupitia mfumo rasmi wa elimu pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali ili kujitegemea kiuchumi.

Mradi huu unatarajiwa kuwanufaisha moja kwa moja wanawake wapatao 209 na wasichana 1,214 kupitia shughuli za utoaji elimu. Aidha, mradi huu unakadiriwa kuwafikia kiujumla watu 2,500 wilayani Longido kwa kipindi chote cha mradi.

Mradi huu unakwenda sambamba na malengo ya maendeleo endelevu ikiwemo lengo namba 1, 4, 5, 8, 10, na 16, ambayo kwa pamoja yanalenga kuondoa umasikini, upatikanaji wa elimu bora, usawa wa kijinsia, kufanya kazi na ukuaji uchumi, kuondoa ukandamizi, pamoja na kujenga misingi ya amani, haki na taasisi imara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

Habari Mchanganyiko

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the love  Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya...

Habari Mchanganyiko

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk....

error: Content is protected !!