Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wanajeshi 600 Urusi wajisalimisha, 1300 Ukraine wauawa
Kimataifa

Wanajeshi 600 Urusi wajisalimisha, 1300 Ukraine wauawa

Spread the love

WAKATI vita kati ya Urusi na Ukraine ikitimiza siku 18 sasa, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amedai kuwa kati ya wanajeshi 500 hadi 600 walijisalimisha kwa wanajeshi wa Ukraine juzi tarehe 11 Machi, 2022.

Aidha, Kiongozi huyo wa Ukraine amesema jumla ya wanajeshi 1,300 wa Ukraine wamepoteza maisha katika vita hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jana tarehe 12 Machi, 2022 jijini Kyiv, Zelensky aliwaonya wanajeshi wa Urusi kuwa hatua yao ya kukamilia miji ya Ukraine ni kwa muda tu.

“Sio rahisi kutawala vichwa na mawazo ya watu… hatua yao ya kukalia miji ni kwa muda tu na wala sio maisha. Nina uhakika wa hilo,” alisema.

Wakati hayo yanajiri, pia imeripotiwa kuwa Uwanja wa ndege wa kijeshi wa Ukraine kusini mwa Kyiv umepigwa kwa makombora ya Urusi.

Meya wa Vasylkiv amesema shambulio hilo liliharibu njia ya ndege na ghala la mafuta, pamoja na kusababisha milipuko katika chumba cha kuhifadhia risasi.

Video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii ilionesha moshi mkubwa mweusi ukifuka kutoka kwenye uwanja wa ndege.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!