Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais mdogo zaidi duniani aapishwa, alimbwaga bilionea
KimataifaMakala & Uchambuzi

Rais mdogo zaidi duniani aapishwa, alimbwaga bilionea

Spread the love

GABRIEL Boric mwenye umri wa miaka 36 ameapishwa jana tarehe 12 Machi, 2022 kuwa Rais mpya wa Chile na kuweka rekodi ya kuwa Rais mdogo zaidi duniani. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Boric ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Chile, alikwaa nafasi hiyo baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika Disemba 20 mwaka jana na kumbwaga mpinzani wake Jose Antonio Kast aliyepata asilimia 44 ya kura zote.

Rais mpya wa Chile, Gabriel Boric (kushoto) akipongezwa na Rais aliyemaliza muda wake Sebastian Pinera ambaye pia ni bilionea

Wakati Boric kupitia Chama chake cha Social Convergence akipata asilimia 56 ya kura zote, hilo lilikuwa mojawapo ya pigo la pili kwa Rais bilionea aliyeondoka madarakani Sebastian Pinera hasa ikizingatiwa aliyetarajiwa kuwa mrithi wake kupitia chama cha Consevative yaani Kast tayari alibwaga.

Hata hivyo, Boric alikuwa mwiba kwa Pinera baada ya kuongoza maandamano ya kumng’oa madarakani mwaka 2019 kabla ya kujitosa katika kinyang’anyiro hicho mwaka jana na kushinda.

Pinera alichukua mikoba ya Urais mwaka 2018 na kukumbuna na maandamano makubwa mwaka 2019 yaliyosababishwa na mdororo wa huduma mbalimbali za kijamii.

Hata hivyo, baada ya Boric kushinda, Pinera aliahidi kumpa ushirikiano katika kipindi cha mpito cha miezi mitatu kabla ya kuapishwa mwezi huu.

AHADI ZAKE KWA CHILE

Katika hotuba yake ya kuapishwa kwa taifa, Rais Gabriel Boric alisema atashughulikia ukosefu wa usawa kati ya raia na wale walioanzisha maandamano ya ghasia mwaka 2019.

Pia alisema kuwa ataboresha sekta ya elimu na kuboresha mfumo wa afya, miongoni mwa mengine mengi.

Pia atafanya mabadiliko makubwa katika jeshi la polisi ambalo limekuwa likilaumiwa kwa kuua mamia ya waandamanaji.

Hatimaye, aliapa kuongeza wigo wa demokrasia ya Chile, wanawake kuwa na haki ya kupiga kura na kugombea nyadhifa mbalimbali.

Boric pia alitoa wito wa mabadiliko katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta, faida za kiuchumi lakini pia kumaliza utofauti unaongezeka kati ya matajiri na maskini.

CHANGAMOTO

Kwa kuwa chama chake hakina wingi wa kura bungeni ikilinganishwa na wapinzani wake kisiasa, Boric atakabiliwa na changamoto katika kutimiza ahadi zake za kurekebisha mfumo wa ushuru na kurekebisha mipango ya pensheni na afya.

Hata hivyo anaonekana si aina ya mtu ambaye anaweza kukimbia majukumu yake kwa sababu ya changamoto.

Aidha, ameweka wazi anataka mabadiliko – kwamba katika baraza lake la mawaziri wanawake ndio watakuwa wengi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

error: Content is protected !!