Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Wakulima walia anguko bei ya Vanila, Serikali yawa bubu
Biashara

Wakulima walia anguko bei ya Vanila, Serikali yawa bubu

Spread the love

LICHA ya Serikali kuhamasisha kilimo kwa ajili ya kuwainua wakulima kipato cha chini, wakulima wa zao la vanila katika kata ya Kanyangereko Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera wamelalamikia kushuka kwa bei ya zao hilo na kuwatisha tamaa. Anaripoti Danson Kaijage, Bukoba. (endelea).

Wakizungumza na MwanaHALISI Online leo wakulima hao wamesema zao hilo licha ya kuwa linalimwa kwa umakini mkubwa mpaka hatua ya kuvunwa bei yake imeshuka ghafla huku serikali ikiwa imekaa kimya.

Mmoja wa wakulima hao ambaye amejitambulisha kwa jina la Robert Mukurasi amesema zao la vanilla mwanzoni lilikuwa likiuzwa kilo moja Sh. 55,000 hadi 70,000 na baadaye likashuka hadi kufikia Sh.35,000 kwa kilo.

“Hadi sasa zao hilo limeshuka kutoka Sh.35,000 kwa kilo na kufikia Sh.3000 kwa kilo moja jambo ambalo linakatisha tamaa na haijulikani sababu za kushuka bei zao hilo.

“Zao la vanilla lilihamasishwa kwa nguvu na wakulima walikuwa na mwitikio mzuri wa kulima zao hilo lakini cha kushangaza kila siku bei inashuka na kuwafanya wakulima kukata tamaa ya kuendelea na kilimo hicho,” ameeleza Mukurasi.

Zao la Vanila

Kwa upande wake Yasini Silaji amabaye naye ni mkulima wa zao hilo amesema kitendo cha mazao yalimwayo katika mkoa wa Kagera kushuka bei bila sababu za msingi kunachangia wakulima wengi kukata tamaa ya kuendeleza mazao hayo.

“Tumekuwa na kilimo cha zao la kahawa lakini bei ilishuka na wakulima wakalazimika kufyeka mibuni yote, zao la majani ya chai nalo ni kama halimsaidii mkulima na sasa zao la vanilla nalo ni changamoto.

“Ikumbukwe kuwa zao la vanilla ni zao linalohitaji utulivu mkubwa tangu kupandwa kwake mpaka inapofikia hatua ya kuvunwa na kuuzwa na wakati mwingine unalazimika kulala shambani ili usiibiwe sasa inapofikia hatua ya kushuka bei bila sababu za msingi nadhani na zao hilo litafyekelewa mbali” ameeleza Mkulima huyo.

Alipotafutwa Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde kuelezea tatizo la kushuka kwa bei ya zao hilo alisema kuwa hawezi kulisemea na ni vyema kumtafuta waziri mwenye dhamana ambaye ni Hussein Bashe.

Alipotafutwa Waziri Bashe ili kufafanua sababu za kushuka kwa zao hilo na hatua zinazochukuliwa na serikali, simu yake iliita bila kupokelewa n ahata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno hakujibu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!