Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kiongozi wa waasi ADF aliyeuawa adaiwa kua Mtanzania
Habari Mchanganyiko

Kiongozi wa waasi ADF aliyeuawa adaiwa kua Mtanzania

Spread the love

JESHI la Uganda limedai kumuua mmoja wa makamanda wa kundi la waasi wa ADF lenye mafungamano na wanamgambo wa dola la Kiislamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa jana Ijumaa imesema, kamanda huyo aliyetambulika kwa jina moja la Fazul, alikuwa raia wa Tanzania na amekuwa akiendesha operesheni katika bonde la Mwalika kwenye mkoa wa Kivu.

Waasi wa ADF wamekuwa wakiendesha shughuli zao kwenye misitu Mashariki mwa Kongo kwa zaidi ya miongo miwili na wamekuwa wakifanya mashambulizi ndani ya nchi hiyo na wakati mwingine nchini Uganda.

Kundi hilo halikutoa taarifa yoyote ya haraka kuhusu kifo cha kamanda huyo. Kampala kwa kushirikiana na jeshi la Congo imekuwa ikipambana na makundi ya wabeba silaha kwa karibu miaka miwili sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!