Saturday , 30 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wadau waombwa kutatua changamoto shule za umma
Elimu

Wadau waombwa kutatua changamoto shule za umma

Spread the love

SERIKALI na wadau wametakiwa kujitoa katika kutatua changamoto zinazokabili shule za umma. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Serengeti iliyopo wilayani Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, Bihimba Nassoro Mpaya, katika mahafali ya sita ya wanafunzi wa darasa la saba shuleni hapo.


Ni baada ya kuipatia shule hiyo vifaa vya kidigitali, vilivyogharimu Sh. moja milioni ikiwemo kompyuta, mashine ya kutokea photocopy na picha.

“Leo mimi nimeguswa na maendeleo ya shule na mimi nawasapoti kwa kuwapa vitendea kazi ili kuwainua wanafunzi. Nafanya hivi kuunga mkono maendeleo yanayofanywa na  Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Bihimba na kuongeza:

“Nawaomba wadau wengine wajitokeze kuisaidia kwa kuwa misaada hii itasaidia watoto wasiokuwa na uwezo.”

Mkuu wa Shule ya Msingi Serengeti, Bhupe Thomas, amesema vifaa hivyo viatsaidia kuimarisha utendaji wa shule yake, huku akiwaomba wadau waendelee kutoa msaada shuleni hapo, ikiwemo kuisaidia ujenzi wa vyoo, uzio na ofisi za awali.

“Tunashukuru tumepoeka vifaa kutoka kwa mwenyekiti wa kamati ambaye ameendlea kujituma na kujitoa mara kwa mara. Hivi vifaa vitatusaidis shule kwa habari ya Mitihani ya majaribio, muhula na kuchapisha kazi zetu za kiofisi,” amesema Mwalimu Thomas na kuongeza:

“Tunaomba Serikali na wadau  waendelee kutusaidia kuboresha miundombinu ya shule, wajitolee kwenye ujenzi wa madarasa na uzio wa shule ili kuisaidia wanafunzi wajifunze vizuri.”


Kwa upande wa Mwalimu wa Shule ya Msingi Serengeti, Catherine Mwageni, amesema vifaa vilivyotolewa na Bihimba viatsaidia kupunguza changamoto ya vitendea kazi kwenye Shule hiyo.

“Tunamshukuru kwa kutuletea vifaa vya kompyuta sababu awali tulikuwa na uhaba wa vifaa. Vifaa hivi viatsaidia wahitaji wasiokuwa na uwezo,” amesema Mwalimu Mwageni.

Katika mahafali hayo, wanafunzi zaidi ya 400 wanatarajia kuhitimu darasa la saba, baada ya kufanya mtihani wa Taifa hivi karibuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Viwanda zaidi ya 200 kuonyesha bidhaa maonyesho ya TIMEXPO Dar

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka...

Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the loveWAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

error: Content is protected !!