Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Wadau wa elimu waililia serikali mtaala wa elimu
Elimu

Wadau wa elimu waililia serikali mtaala wa elimu

Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu
Spread the love

WADAU wa elimu nchini wamehoji walimu kutoshirikishwa katika mchakato wa kuandaa mtaala wa elimu mwaka 2016, kabla ya serikali kuupeleka mashuleni. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wakichangia katika mada iliyohusu mtazamo wa walimu kuhusu Mtaala wa elimu wa mwaka 2016, wadau hao walihoji ni kwanini umekuwa na sintofahamu nyingi huku wakitaka kujua ni kwanini  haukuwashirikisha walimu kabla ya Serikali kuupeleka mashuleni.

Wadau hao walikuwa katika mkutano wa siku tatu uliandaliwa na  Mtandao wa Elimu Tanzania Ten/Met kujadili ubora wa elimu nchini.

Akiwasilisha mada hiyo, Mshauri wa Elimu kutoka Haki Elimu, Wildaforce Maina, alisema katika utafiti alioufanya mwaka 2018, amegundua kwamba walimu wengi hawana uelewa kuhusiana na mtaala wa elimu wa mwaka 2016.

“Nilifanya utafiti wangu mwaka 2018 na nilichogundua ni kwamba walimu wengi hawana uelewa kuhusiana na mtaala wa mwaka 2016 wengi wameukuta wakati wa kufundisha tu hawajui ukoje hivyo wamekuwa wakifundisha tu bora liende,” alisema.

Mshauri huyo wa elimu aliishauri Serikali kuwashirikisha walimu pindi ambapo kunakuwa na mabadiliko ya mitaala ili iwe rahisi kujua changamoto zipi ambazo zipo kwa walimu pamoja na wanafunzi.

Kwa upande wake, Meneja Program, kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAPIE), Laurent Gama alisema mtaala wa elimu wa mwaka 2016 ulitangulia darasani kabla ya walimu hawajaujua unataka nini.

“Rai yangu mabadiliko lazima yaendane na mahitaji lazima kuwe na vifaa vya utekelezaji, vifaa visichelewe kama ambayo mtaala unataka, lazima kuwe na usimamizi mzuri, lazima kuwe na vitabu, lakini ni lazima walimu wapate mafunzo,” alisema.

Naye, Mtaalamu wa elimu kutoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Peter Mlimahadala alisema mitaala walimu kutoijua mapema inaathari kubwa kwa taifa kwani wanafunzi wanaozalishwa wanakuwa hawana  ubora unaotakiwa.

“Walimu wao ndio wanaweza kueleza changamoto kwa sababu ndio wanaofundisha wao ndio wanatakiwa kutoa ushauri tunatakiwa tufundishaje, hili ni muhimu sana kwa taifa letu baadae tutakuwa na wataalamu ambao ni jina tu,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kufumua mitaala ya vyuo vikuu, ufundi stadi

Spread the loveSERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

error: Content is protected !!