April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wizara ya Elimu yaingilia kati ukata wa mikopo UDSM

Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu

Spread the love

WIZARA ya Elimu imeagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB),  kukutana na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ili kupata suluhu ya changamoto ya mikopo ya wanafunzi wa chuo hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 16 Disemba 2019 na wizara hiyo, kupitia ukurasa wake wa Twitter, siku moja baada ya Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa UDSM (DARUSO) kutoa saa 72 kwa HELSB, kutatua changamoto hiyo.

Wizara hiyo imeagiza HESLB na uongozi wa chuo hicho, kukutana na DARUSO leo, ili kutatua changamoto hizo.

Aidha, Wizara hiyo imewasihi wanafunzi wa chuo hicho kuwa watulivu na kuendelea na masomo yao, wakati changamoto zao zikishughulikiwa.

Jana tarehe 15 Disemba 2019, DARUSO ilitoa saa 72 kwa HESLB kutoa mikopo kwa wanafunzi, kurudisha fedha za mikopo za wanafunzi, ilizokata. Pamoja na kuwapangia mikopo wanafunzi wa mwaka wa kwanza, ambao rufaa zao zilitupingwa, huku wakiwa ni wahitaji wa mikopo hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali hiyo kulalamika kwamba, kumekuwa na changamoto ya wanafunzi wanaondelea na masomo kutopewa mikopo, na wengine kukatwa fedha zao za mikopo.

error: Content is protected !!