Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO
Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Rais wa Urusi, Vladimir Putin
Spread the love

SERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake, ili kujihami na vitisho vya kiusalama, kufuatia kupanuka kwa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Wizara ya Ulinzi ya taifa hilo, imesema Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ametia saini amri ya kuongeza idadi ya wanajeshi 170,000 ili kufikia 1,320,000, sawa na ongezeko la asilimia 15.

Mtandao wa BBC Swahili umeripoti kuwa, uamuzi huo unatokana na ongezeko la nchi jirani za Urusi, kujiunga na NATO, ikiwemo Finland iliyojiunga hivi karibuni, baada ya Urusi kuanzisha operesheni ya kijeshi nchini Ukraine, ikipinga uamuzi wake wa kuomba kujiunga na jumuiya hiyo.

Katika taarifa yake, Wizara ya Ulinzi Urusi imedai taifa hilo linakumbwa na vitisho vya kiusalama, kutokana na ongezeko la vikosi vya kijeshi vya NATO, karibu na mpaka wake.

Urusi imekuwa ikipinga majirani zake kujiunga na NATO kwa madai kuwa hatua hiyo inahatarisha usalama wake kwa kuwa ni sawa na kukaribisha miundombinu ya kijeshi ya jumuiya nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!