Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel
Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the love

MUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai wake, baada ya kujichoma moto kwa kutumia mafuta ya petroli, nje ya ubalozi mdogo wa Israel nchini Marekani, akipinga vita kati ya taifa hilo na kundi la wanamgambo la Hamas, kutoka Palestina. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Mkuu wa Polisi wa Mji wa Atlanta nchini Marekani, Darin Schierbaum, amesema tukio hilo lililotokea jana Ijumaa, limesababishwa na maandamano ya kisiasa.

Mbali na muandamanaji huyo, mlinzi mmoja aliyejaribu kumwokoa naye ameripotiwa kupata majeraha baada ya kuungua mkononi.

Naibu Balozi wa Israel, Kusini-Mashariki mwa Marekani, Anat Sultan-Dadon, amesema Israel inasikitishwa na tukio hilo ambalo amedai lkinaonyesha chuki dhidi ya taifa lake.

Tukio hilo limetokea baada ya Israel kuaghiri mpango wake wa kusitisha mapigano na kuyarejesha katika ukanda wa Gaza, ikidai Hamas imeshindwa kutekeleza makubaliano ya kusimamisha vita na kuacha mateka wote wa Israel.

Hamas inadaiwa kuanzisha mashambulizi katika kipindi ambacho pande zote mbili zimekubaliana kusitisha ili kutoa nafasi ya pande zote mbili kuwaacha huru mateka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!