Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Umemsikia Mayele, hana wasiwasi na Al Hilal
Michezo

Umemsikia Mayele, hana wasiwasi na Al Hilal

Fiston Mayele, mshambuliaji wa Yanga
Spread the love

 

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga, Fiston Kalala Mayele ameonekana kutokuwa na wasiwasi na mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal kutoka Sudan Kusini, huku akisisitioza kuwa timu yake itafuzu hatua ya makundi. Anaripoti Damas Ndelema….(endelea)

Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, watacheza na wasudani hao mara baada ya kuvuka kwa kishindo kwqa mchezo wa hatua ya awali kwa kuwafumua Zalan FC k,utoka Sudan Kusini jumla ya mabao 9-0, katika michezo yote miwili.

Akizungumza kwenye moja ya mahojiano na televisheni ya hapa nchini, Mayele alisitizxa kusema kuwa kwa sasa klabu yake ya Yanga inawachezaji wakubwa ambao wanaweza kuimili presha za michezo hiyo.

“Sisi kama wachezaji hatujapata presha yoyote, Yanga tunawachezaji wakubwa tunashazoea ile presha, mwaka wa kwanza kucheza kimataifa ilikuwa nilivyokuwa As Vita, kwa hiyo tumezoea” Alisema Mayele

Kwenye hatua hiyo, Yanga itaaznia nyumbani, kati ya Oktoba 8 au 9 mwaka huu, jijini Dar es Salaam kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Kuelekea mchezo huo wa nyumbani mshambuliaji huyo amesema kuwa, watajitahidi kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo ili wapate uraisi wa kufuzu kwenye mchezo wa ugenini utakaopigwa nchini Sudan.

“Sisi tutajitahidi mechi ya kwanza tupate matokeo mazuri n akule kwao tutaenda kujitahidi ili tuingia makundi.” Alisema mshambuliaji huyo

Kwenye ushindi wa mabao 9 ambao Yanga waliupata dhidi ya Zalan FC, Mayele alipachika jumla ya mabao sita, huku kila mcxhezo akifunga mabao matatu.

Kama Yanga itafanikiwa kufuzu kwa hatua ya makundi itakuwa imefanikiwa kufanya hivyo amara baada ya kupita kipindi cha miaka 24, ambapo kwa mara ya mwisho Yanga ilifuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika 1998.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!