Rais wa Kenya, William Ruto amesema serikali ya Ukraine inapanga kuweka kituo cha nafaka mjini Mombasa kama sehemu ya hatua kubwa ya kukabiliana na uhaba wa chakula nchini Kenya na maeneo mengine ya Afrika Mashariki. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea)
Ruto ambaye alikutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy pembezoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York nchini Marekani jana Jumanne alisisitiza uungaji mkono wake wa suluhu la amani kwa mzozo wa Russia na Ukraine.
“Huko New York, Marekani nilifanya mazungumzo na Rais wa Zelensky ambaye aliazimia kuanzisha kituo cha nafaka katika Bandari ya Mombasa ili kukabiliana na uhaba wa chakula Afrika Mashariki,” Ruto alisema.
“Kenya inatetea utatuzi wa amani wa mzozo wa Urusi na Ukraine ili kurejesha utulivu, kupunguza mateso ya watu na kukomesha uharibifu wa mali,” aliongeza.
Leave a comment