Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Kagame kuwania muhula wa nne
Kimataifa

Rais Kagame kuwania muhula wa nne

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Spread the love

Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema atawania muhula wa nne katika uchaguzi wa rais mwaka ujao. Anaripoti Matilda Peter kwa msaada wa Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

“Ndiyo, hakika mimi ni mgombea,”Kagame aliambia jarida la lugha ya Kifaransa la Jeune Afrique jana Jumanne.

Alipoulizwa kuhusu nchi za Magharibi zitachukulia vipi uamuzi wake wa kugombea tena, Kagame alisema, “Samahani kwa nchi za Magharibi, lakini kile ambacho nchi za Magharibi hufikiri si tatizo langu”.

“Nimefurahishwa na imani ambayo Wanyarwanda wanayo kwangu. Nitawatumikia daima, kadri niwezavyo,” aliongeza Kagame

Kagame alitania mwezi Aprili kwamba anatazamia kustaafu na kukabidhi madaraka baada ya miaka 23 madarakani.

Chama tawala nchini humo, Rwandan Patriotic Front (RPF-Inkotanyi), kilimuacha Kagame kuendelea kuhudumu kama mwenyekiti wake mwezi Aprili. Ameongoza chama hicho tangu 1998.

Kagame amekuwa rais wa taifa hilo la Afrika Mashariki tangu mwaka wa 2000. Kura ya maoni iliyozua utata mwaka 2015 iliondoa ukomo wa mihula miwili ya kikatiba kwa marais.

Alishinda uchaguzi uliopita wa 2017 kwa asilimia 98.8 ya kura.

Rwanda chini ya Rais Kagame imekuwa na utulivu wa kisiasa lakini wakosoaji na makundi ya haki za binadamu yanaituhumu serikali yake kwa kuweka mipaka ya uhuru wa kisiasa na kukandamiza upinzani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Sakata la uhamiaji Rwanda lamng’oa waziri Uingereza

Spread the loveWaziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Robert Jenrick amejiuzulu baada ya...

Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the loveMUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai...

Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Spread the loveSERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake,...

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

error: Content is protected !!