Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara Watumiaji mtandao wa X sasa kulipia huduma
Biashara

Watumiaji mtandao wa X sasa kulipia huduma

Spread the love

MMILIKI wa mtandao wa kijamii  X, Elon Mask ambao zamani ulikuwa unaitwa Twitter anatarajiwa kuweka tozo za malipo katika utumiaji wa mtandao huo. Anaripoti Mlelwa Kiwale, TUDARCo kwa msaada wa Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kwa mujibu wa Mask watumiaji wote wa mtandao X wajiandae kuanza kulipia  ili kuweza kupata huduma hizo.

“Tunaelekea kuwa na malipo madogo ya kila mwezi kwa matumizi ya mfumo,” amesema mmiliki wa Tesla na SpaceX.

Musk amekuwa akisema kitu hicho kwa muda mrefu kuwa suluhisho lake la kuondoa roboti na akauti ghushi kwenye jukwaa la mtandao huo ni kutoza ada kwa watumiaji wake ili kuwapa vipengele vyenye machapisho marefu na kuongezeka kwa muonekano wa kipekee katika mtandao huo.

Hata hivyo, katika huduma hizo zilizoboreshwa kwa kulipia kwa mfumo wa X Premium  bado kuna watumiaji wanaoweza kutumia mtandao huo bila malipo.

Mpango hho umeungwa mkono Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ambaye alisema mfumo wa malipo ndiyo njia pekee ya kukabiliana na utumizi wa akaunti zinazoendeshwa na roboti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cheza sloti ya Zombie Apocalypse na ushinde kirahisi

Spread the love Wengi wetu hupenda filamu za Mazombie huwa zinatishakidogo lakini...

Biashara

Ushirikishwaji wa wafanyakazi ni muhimu katika utekelezaji wa sera za afya na usalama kazini

Spread the love  KILA ifikapo Aprili 28 ya kila mwaka, dunia huadhimisha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Biashara

Wazir Jr kinara wa ufungaji KMC FC ajiunga Meridianbet

Spread the love    MUITE Wazir Jr ‘The King of CCM Kirumba’,...

error: Content is protected !!