JESHI la Polisi limesema limeona video fupi (clip) ikimwonesha Mtoto aliyefanyiwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji. Anaripoti Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi, Dodoma … (endelea).
Akitoa taarifa hiyo msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi, SACP David Misime amesema Jeshi hilo limeanza kuifanyia kazi kuanzia ilipoanza kusambaa ili aliyefanya kitendo hicho cha kinyama kisichokubalika aweze kukamatwa na hatua zingine za kisheria ziweze kufuata.
Misime ameongeza kuwa mtoto huyo lazima atakuwa na Mama, Babu, Bibi, Shangazi, Mjomba, Majirani na Viongozi wa Serikali za Mitaa ambapo ameomba ushirikiano wa karibu ili hatua za kisheria kisheria zichukue Mkondo wake.
Msemaji wa Jeshi hilo ametoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za aliyefanya kitendo hicho au mahari kilipo tokea asisite kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi au kwa Kiongozi yeyote yule ili kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa.
Leave a comment