Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Muhongo aanika miradi ya maendeleo Musoma
Habari za Siasa

Prof. Muhongo aanika miradi ya maendeleo Musoma

Spread the love

 

OFISI ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospster Muhongo, imeishukuru Serikali na wadau wa maendeleo kwa kufanikisha ujenzi wa miradi ya maendeleo mbalimbali unaoendelea jimboni humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Shukrani hizo zimetolewa na ofisi hiyo leo tarehe 19 Septemba 2023, wakati ikielezea hatua mbalimbali za ujenzi wa miradi ya maendeleo inayoendelea Musoma Vijijini, mkoani Mara.

Kwenye sekta ya mawasiliano, taarifa hiyo imesema ujenzi wa barabara ya Musoma-Makojo-Busekera, unaofanyika kwa awamu mbili, unaendelea ambapo uko katika taratibu za manunuzi kwa ajili ya uwekaji lami.

“Utengenezaji wa barabara la Musoma-Mugango-Makojo-Busekera, TANROADS mkoa wameanza matengenezo ya uboreshaji wa barabara hili kwa kipande cha Musoma-Mugango,” imesema taarifa ya ofisi hiyo.

Mradi mwingine unaondekea jimboni humo ni wa kilimo cha umwagiliaji, ambapo upembuzi yakinifu umeanza kufanyika kwa ajili ya kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika Bonde la Bugwema na Bonde la Suguti.

Kwa upande wa sekta ya elimu, miradi inayojengwa ni ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi katika shule za sekondari , pamoja na miundombinu muhimu itakayowezesha shule hizo kufundisha masomo ya kidato cha tano na sita.

“Vinavyohitajika kwa uanzishwaji wa “science high school” ni maji ya bomba, maabara 3, bweni, na bwalo la chakula. Lengo letu ni 2024, jimbo letu liwe na angalau high school mbili au tatu za masomo ya sayansi ile ya Kasoma ni ya masomo ya sanaa,” imesema taarifa.

Pia, Serikali kupitia mradi wa Boost, imetoa Sh. 1.35 bilioni kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu katika shule za msingi tisa jimboni humo.

Taarifa ya jimbo hilo imesema, miradi mbalimbali ya maji inaendelea kujengwa ikiwemo ya usambazaji kutoka Ziwa Victioria, ujenzi wa visima na matanki.

Miradi ya maendeleo inayojengwa katika sekta ya afya ni pamoja na ujenzi wa zahanati 14.

“Hospitali ya Halmashauri yetu yenye hadhi ya Hospital ya Wilaya imeanza kutoa huduma za afya hapo ilipojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti. Hospitali hii inavyo vifaa tiba vya kisasa sana, ikiwemo Digital X-ray, Ultrasound, Vifaa vya Upasauji, Mitambo ya kutengeneza Oxygen,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!