October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

UDSM yafadhili walimu 16 kufundisha masomo ya sayansi

Spread the love

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kupitia Ndaki ya Sayansi Tumizi na Sayansi Asili (CoNAS), kimewezesha wanafunzi 16 waliohitimu masomo ya ualimu ya sayansi kufundisha shule nne za jijini Dar es Salaam. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea)

Hayo yamesemwa jana Septemba Mosi 2022 na Mkuu wa Ndaki ya CoNAS, Profesa Flora Magige wakati akizungumza na wanufaika wa Program ya Hisabati na Masamo ya Sayansi yakiwemo fizikia, kemia na biolojia ambao walikuwa wakipatiwa mafunzo ya namna ya kwenda kufundisha.

Prof. Magige amesema wameamua kuna na program hiyo ili kuongeza idadi ya walimu wa vyuo vikuu kufundisha masomo ya sayansi ambayo yamekuwa na idadi ndogo ya wanafunzi.

Mkuu huyo wa ndaki amesema program hiyo imeanzishwa mwaka jana na imeonesha matokeo chanya kwa wanafunzi wa shule husika.

“Tumeanzisha program hii ya hisabati, fizikia, kemia na biolojia ambapo Shule za Sekondari za Salma Kikwete, Mugabe, Yusuph Makamba na Manzese zimenufaika,” amesema.

Amesema walimu ambao wamepata nafasi hii ni wale ambao wamefaulu vizuri katika masomo husika, hivyo amewataka wanufaika hao kuzingatia maadili ya utumishi wa umma katika kazi hiyo.

Prof.Magige amesema programa hiyo ni endelevu kwa walimu wa masoko hayo na kwamba mkakati ni kupanua wigo wa maeneo ikiwemo Zanzibar na mikoani.

Mratibu wa program hiyo, Dk Ally Mahadhy amesema wameamua kuja na program hiyo ili kuhakikisha lengo la kuzalisha wanasayansi wengi linafanikiwa, ili Tanzania ya viwanda iweze kutekelezeka.

Dk Mahadhy amesema UDSM ina majukumu matatu makubwa ambayo ni kufundisha kufanya tafiti na kutoa huduma kwa jamii hivyo program hiyo inajikita katika kutoa huduma kwa jamii.

“Tunachofanya hapa ni sehemu ndogo ya kutatua tatizo la walimu wa hisabati na masomo ya sayansi, hivyo tunaviomba vyuo vingine kuwa na program kama hii, ili lengo la Tanzania ya viwanda liweze kufikiwa,” amesema.

Mratibu huyo amesema wanatamani kutoa ufadhili kwa walimu wengi ila changamoto kubwa ni rasilimali fedha, hivyo kuwaomba wadau wengine kuwezesha.

Mhadhiri huyo ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhamasisha watoto wao kusoma masomo ya hisabati na sayansi ili kuwezsa kukabiliana na uhaba wa wataalam wa maeneo hayo.

Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Hisabati UDSM, Dk Saisd Sima amewataka walimu hao kuzingatia maadili, lugha, nidhamu, mazingira na mavazi yenye heshima wakiwa kazi.

“Nimewaambia wajikite katika maadili ya ualimu, ili waweze kutengeneza wasifu mzuri katika utumishi wao,” amesema.

Dk Mwingereza Kumwenda amesema katika kuhakikisha walimu hao wa muda wanafanya vizuri katika program hiyo watakuwa wanawafuatilia kwa karibu.

Kumwenda ambaye ni mwalimu wa fizikia amesema wanatarajia kuona waalimu hao wanakiwakilisha chuo vizuri katika ufundishaji ili kuvutia wanafunzi wengi kuendelea kukitumia kupata elimu ya juu.

Kwa upande wake Mwalimu wa Hisabati Halima Mohammed na Mwalimu Faustine Elius wa Biolojia wamesema programa hiyo imekuja wakati muafaka na kuahidi kufanya kazi kwa weledi ili lengo la chuo na jamii liweze kutimia.

error: Content is protected !!