Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia azindua kituo kipya cha Polisi Kizimkazi
Habari za Siasa

Rais Samia azindua kituo kipya cha Polisi Kizimkazi

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo tarehe 2 Septemba, 2022 ameanza ziara visiwani Zanzibar ambapo pamoja na mambo mengine amezindua kituo kipya cha polisi Kizimkazi katika jimbo la Makunduchi Wilaya ya Kusini. Anaripoti Juliana Assenga UDSM) …. (endelea)

Akizungumza katika uzinduzi huo Rais Samia amesema kituo hicho kimejengwa kisasa kwa kuzingatia mahitaji yote muhimu ya kibinadamu.

Rais amesema kituo hicho kitaweza kuwarahisishia wananchi na polisi kutotumia muda mrefu kumkamata mhalifu mara tu wapatapo taarifa, na kuwa kitaweza kusaidia katika kuweka ulinzi na usalama katika eneo la Kizimkazi.

Rais ameipongeza polisi kwa kuweza kufuata maelekezo aliyokwisha yatoa alipokuwa mkoani Kilimanjaro juu ya matumizi mazuri ya fedha kwa kuweza kutumia vizuri fedha zilizopo katika mfuko wa polisi zilizosaidia kujenga kituo hicho .

Rais ameitaka Polisi kuweza kuiga mfano wa ujenzi wa kituo hicho cha Kizimkazi, kwani licha ya kujengwa kituo hicho pia zipo nyumba za polisi zilizojengwa kwa ukaribu kwa ajili ya kuweza kuimarisha ulinzi na usalama wa eneo hilo.

Rais pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano mkubwa kwa polisi katika kuweza kufanikisha na kuhakikisha ulinzi usalama kwa eneo hilo unaimarika.

Kwa upande wake Waziri wa mambo ya ndani na nje ya nchi, Hamadi Massauni, amemshukuru Rais Samia kwa kuweza kutenga kiasi cha hela kuingia katika mfuko wa polisi ambao ndio ulioweza kusaidia katika kufanikisha ujenzi wa kituo hicho cha polisi cha Kizimkazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!