Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wawekezaji Arusha wampongeza Samia ujenzi barabara za TARURA
Habari Mchanganyiko

Wawekezaji Arusha wampongeza Samia ujenzi barabara za TARURA

Spread the love

WAWEKEZAJI na wananchi wa kata ya Themi, Halmashauri ya Jiji la Arusha wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwajengea kwa kiwango cha lami barabara za Themi -Viwandani zenye urefu wa kilometa 1.4 kwa gharama ya shiligi bilioni 1.1. Anaripoti Mwandishi Wertu … (endelea).

Pongezi hizo zimetolewa katika ya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja jijini Arusha iliyofaywa na bodi ya ushauri ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA).

Akitoa pongezi hizo mkurugenzi wa “Spanish Tiles” Bobby Chadha alisema anamshukuru Rais Samia kwa kuwajali na kuwapatia barabara nzuri na bora za lami maeneo ya viwandani.

“Kwa mara ya kwanza tumepata barabara hizi za lami kwa zaidi ya miaka 40 niliyokuwa. Barabara hizi zitasaidia kupungza gharama za usafiri, kukuza biashara na pia kupendezesha mji,” alisema Bobby.

Naye Satbir Hanspaul mkurugezi mtendaji wa “Hanspaul Group” alisema walikuwa wanapata changamoto kwa magari kufika viwandani na magari mengi yalikuwa yanaharibika lakini sasa barabara imewaondolea kero hizo.

“Wageni walikuwa wakija eneo la Kiwanda na kuona miundombinu mibovu walikuwa wanapata wasiwasi na kiwanda pia, lakini tumeona Serikali yetu imeona changamoto na kuifanyia kazi haraka, sasa tunaaminika kwa sababu mazigira yameboreshwa,” alisema Hanspaul.

Mama Veronica Saimon mfanyabiashara wa eneo la viwandani alisema kuwa kabala ya barabara haijajengwa walikuwa wakipata shida kutokana na vumbi jingi pamoja na matope wakati wa mvua hali iliyokuwa inaathiri biashara yao.

Alieleza kwa sasa wanafanyabishara bila shida na wateja wengi wanawapata baada ya barabara kujengwa.

Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo (CCM) aliwashukuru watendaji na wataalamu wa TARURA kwa kazi kubwa wanayofanya na ameona tofauti kubwa sana baada ya TARURA kuanzishwa.

“Huko nyuma kaba ya kuanzishwa TARURA ilikuwa ngumu kupeleka mradi sehemu inayoeleweka na ukaleta tija kwa sababu kila diwani alikuwa akivutia upandewa wake. Leo mmewasikia hapa wawekezaji wamesubiri barabara kwa takribani miaka 40 lakini baada ya TARURA kuanzishwa barabara imejengwa,’alisema Mhe. Gambo.

Aidha alimshukuru Rais Samia kwa Kuendelea kuenzi falsafa ya Serikali ya “Tanzania ya Viwanda” kwa kuboresha miundombinu katika maeneo hayo ya viwandani yenye viwanda zaidi ya 20, ambapo ajira zinaogezeka na uchumi wa wanachi wa maeneo ya viwandani wanaofikia takribani 11,000 unaboreka.

Mtendaji mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff kwa upande wake alisema kuwa wamejipanga kuwafikia wannachi katika sehemu ambazo hazifikiki na pia katika maeneo ya kimkakati.

“TARURA tunakufikisha kusikofika lakini nasema pia Penye nia pana njia na pasipo na njia TARURA tupo, “alisema Mhandisi Seff.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!