Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari Simba Queen wapewa basi kwa Safari za ndani
HabariMichezo

Simba Queen wapewa basi kwa Safari za ndani

Spread the love

 

Timu ya Soka ya wanawake ya Simba (Simba Queens) leo  Septemba 2 2022 imepewa basi na kampuni ya  uuzaji wa magari ya Africarriers kwa ajili ya matumizi ya Safari za ndani ya nchi kwa timu hiyo ya wanawake ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya mkataba baina ya pende zote mbili. Anaripoti Damas Ndelema ………..(endelea)

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyo hudhuriwa na waandishi wa habari yaliyofanyika kwenye Ofisi za kampuni hiyo Vingunguti jijini Dar es Salaam mkuu wa Rasilimari watu wa Africarriers Lydear Gorge amesema kuwa lengo la kampuni yao ni kuiunga mkono serikali katika ya Tanzani katika kukuza mpira wa hapa nchini na wao wameanza kwa kwa kuipa nguvu Simba queens kulingana na matakwa ya mkataba unavyosema

“lengo letu ni kuisapoti mpira wa Tanzania kama ilivyo kwa serikali na Shirikisho la soka nchini (TFF) tulikubaliana kuwapa mabasi na leo tunakabidhi gari la pili kwa Simba Queens” alisema Mkuu huyo wa Rasilimali watu

Aidha hii inakua kama motisha kwa Simba Queens ambao hivi karibuni wametoka kutwaa ubigwa wa timu za wanawake upande wa CECAFA ambalo lilipata udhamini kutoka kwa  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na  kutambulika kama ( SAMIA CUP) hivyo Simba queens kupata tiketi ya kwenda kuiwakilisha inchi katika michuano ya Klabu bigwa Afrika kwa upande wa wanawake ambayo yatafanyika nchini Morocco mwaka huu.

Kwa upande wa klabu ya Simba ambao waliwakilishwa na mtendaji mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez alisema kuwa, kikosi hiko kitakwenda kuiwakilisha nchi vizuri miezi miwili ijayo na wadhamini hao wamefanya kitu kikubwa kama walivyoahidi.

“Simba queen sasa inaenda kimataifa zaidi Kwa kuiwakilisha nchi kwenye Ligi ya mabingwa, licha ya Aficarrier kutupatia basi hilo, lakini bado tupo kwenye mzungumzo ili waje kama wadhamini wakuu wa timu hii” Alisema kiongozi huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!