Klabu ya soka ya Simba ya Jijini Dar es Salaam leo Septemba 2 2022 imepata pigo baada aliyekuwa daktari wa timu ya wakubwa ya wanaume ambaye kwa sasa alikuwa daktari wa timu ya vijana Yassin Gembe amefariki leo mchana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Anaripoti Damas Ndelema…..(endelea)
Taarifa hiyo imetolewa kwenye ukrasa maalimu wa Simba kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kuthibitisha msimba wa daktari huyo aliyekuwa akihudumu katika timu ya vijana ya wanaume ya Simba baada ya kuhudumu kwenye timu ya wakubwa kwa kipindi kirefu
https://twitter.com/SimbaSCTanzania/status/1565661898858762240
“kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha aliyekuwa daktari wa timu ya wanaume (seneor Team) ambaye kwa sasa alikuwa daktari wa timu ya vijana(youth Team) Dkt. Yassin Gembe ambacho kimetokea leo mchana kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili” Ilisema taarifa hiyo
Aidha hili ni pigo kwa wanamichezo na jamii kwa ujumla kutokana na uwajibikaji aliokuwa akiuonesha Daktari huyo wakati akihudumu katika tasinia ya michezo enzi za uhai wake kwani amehudumu kwenye klabu ya simba kwa kipindi cha zaidi ya miaka nane kwa mafanikio makubwa kabla mauti hayajamkuta
Leave a comment