Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Tatizo umasikini au CCM?
Makala & Uchambuzi

Tatizo umasikini au CCM?

Viongozi wa CCM wakiongoza Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM
Spread the love

UMASIKINI katika jamii si msamiati mgeni, hasa wakati huu ambapo kumekuwepo na jitihada mbalimbali za kitaifa na za kimataifa za kuuangamiza. Anaandika Mbonea Mkasimongwa…(endelea).

Wanasosholojia wanasema ili mtu apate mafanikio katika tatizo linalomsibu, lazima ajitambue. Hivyo kila anayeshiriki kutokomeza umaskini ajue maskini ni nani?

Swali la msingi hapa serikali inatatambua tatizo hilo? Inalitambuaje? Je, inajua kuwa serikali ina mchango mkubwa wa kuliondoa? Nchi yetu ipo huru tangu mwaka 1961 chini ya TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kuna vipimo viwili vya kutambua aliye maskini. Kipimo cha kwanza ni kile cha kimataifa ambacho kinasema, “Yeyote mwenye kipato cha chini ya dola moja ya Marekani kwa siku anahesabika kuwa maskini. Tanzania dola moja hivi sasa ni sawa na shilingi 2300. Hivyo kwa mwenye kipato kama hicho anatambulika ni masikini.

Kipimo kingine ni kile ambacho hutumiwa na wataalamu wengi wa uchumi hapa nchini kumtambua maskini ni kile cha kujipatia mahitahi ya lazima ambayo ni chakula, malazi na mavazi.

Kwa upande wa chakula, huangaliwa iwapo kaya ina mudu milo mitatu kwa siku. kama hawapati huhesabiwa ni
masikini wa kutupwa.

Kwa upande wa malazi huangaliwa nyumba wanayoishi wanafamilia. Kama haina faragha wala choo, wanajibanza kwenye chumba kimoja au hulala nyumba pamoja na mifugo, haina madirisha yanayoingiza hewa ya kutosha ama imeezekwa kwa majani. Wanakaya wanaoishi kwenye nyumba hizo huitwa
ni maskini hohe hahe.

Mavazi nayo hutumika kama moja kipimo cha kumtambua maskini. Familia zinaposhindwa kuwa na nguo safi, zinazofuliwa kila mara na kunyooshwa pasi nazo hungizwa kwenye kundi la watu maskini. Ni dhahiri familia zinapokosa kipato cha kukidhi mahitaji hayo ya lazima hukosa ziada ya elimu ya watoto afya na maji safi.

Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini. Umaskini wa nchi hupimwa kutokana na ukubwa wa pato la taifa kwa mwaka (GDP), matumizi ya kiwango cha chini cha teknolojia, uduni wa huduma za jamii, madeni, miundombinu hafifu, upatikanaji wa maji safi na salama na uwezo mdogo uzalishaji katika kilimo na viwanda.

Kutokana na vipimo hivyo ni dhahiri nchi na watu wake ni maskini. Uwe umaskini wa kipato kwa wanawake na wanaume na umaskini kama nchi.

Tanapaswa kujiuliza, kwanini mpaka sasa bado tunashindwa kupunguza umaskini. Mojawapo ya sababu inayotukwamisha kuondokana na umaskini ni mtazamo.

Umasikini wa kifikra unawafanya Watanzania wengi kugopa kuingia katika shughuli za maendeleo. Mathalani mtu ana shamba kubwa lenye miti badala ya kupata utaalamu wa kufuga nyuk6i ili azalishe asali, anaona bora anunue shoka ili akate mkaa. Ukataji mkaa ni sulba kubwa na haina tija na kipato chake ni kidogo

Kubadili fikra (Mindset) kunakuja baada ya kujitambua, hivyo kwa vile wengi hufikiria umaskini ni maumbile mara zote katika kupambana na vita dhidi ya adui huyo huendeshwa mambo kwa mazoea ya nyuma. Umaskini wa kifikra husababisha wananchi wengi kutokujitambua na kutambua mustakabali mzima wa maisha yao.

Wengi hukosa upeo wa utambuzi, jambo hili husababisha kutopata tija au ufanisi kidogo katika shughuli za utafutaji riziki. Chanzo au asili ya umasikini ni tukio la kihistoria.

Tangu enzi za mambabu zetu, wageni walipoingia waliona nchi yetu ilivyo na raslimali nyingi yakiwemo madini ardhi yenye rutuba na mbuga za wanyama.

Kuna mito, bahari na maziwa makubwa, vivutio vya dunia kama vile Mlima Kilimanjaro na nyinginezo lukuki. Simulizi zinasema babu zetu walitumia madini kama kete za kuchezea bao, milima kama sehemu za matambiko. Baada ya ujio wa wageni wazee wetu walitoa dhahabu kwa kubadilishana na kioo cha kujitazama.

Toka wakati ule hadi leo karibu miaka 57 ya uhuru bado tumeshindwa kuwa na mikakati ya kuzitumia raslimali hizo ili kuinua ustawi wa taifa. Tunaambiwa na watengeneza sera kuwa kutokana na uduni wa teknolojia, mitaji na utaalamu wa kutosha sasa tumewakaribisha wawekezaji wageni kuchimba nasi kuambulia kiduchu baada ya mwekezaji kutoa gharama za uchimbaji.

Licha ya kuwa na ardhi yenye rutuba, maji ya kutosha kwa ajili ya
kilino cha umwagiliaji, nchi yetu imekuwa inakabiliwa na upungufu wa chakula kila mara na kusababisha kutumia akiba ya fedha za kigeni tunazozipata kwa njia ya kudunduliza kununua chakula kutoka nchi za nje ili kupambana na njaa.

Umaskini unatutumbukiza katika uharibifu wa mazingira, uchomaji moto misitu, ufugaji wa mifugo na uwindaji haramu unaharibu uoto wa asili na hali oevu.

Kilimo cha jembe la mkono huku kikitegemea mvua
kinatukosesha mazao ya chakula na biashara. Hali hiyo pia husababisha ukame na hivyo serikali hulazimika kukopa

Kwa upande wa nguvu kazi kama taifa tumeshindwa kujenga tabia za vijana katika kupenda kazi na hasa za uzalishaji mashambani, viwanda na migodini.

Vijana wengi wamejikita kwenye uchuuzi na wengi mijini
hupenda kukaa vijiweni huku wakisogoa na wakati mwingine kuilalamika serikali kuwa hakuna ajira

Tulitegemea makundi ya vijana wanaomaliza masomo katika vyuo na shule mitaala yake ingeelekezwa katika utatuzi wa matatizo wangeweza kubuni miradi midogo midogo na kupata mitaji ya kuendeleza miradi hiyo ili wajikwamue na umaskini. Wangeimarisha masoko na kuongeza thamani ya mazao wazalishayo.
Wanasiasa wetu wamekuwa na kauli mbiu zinazopokelewa katika hali hasi mathalani kauli isemayo “ Kina mama tukiwezeshwa tunaweza” akina mama wengi sasa hawafanyi kazi kwa kudai kuwa, hawajawezeshwa. Hata hao wengine wanapopatiwa mikopo hutumia kununulia mapambo ya mwilini, nguo na vipodozi

Wengine hutumia mikopo kwa ajili ya kuandaa hafla mbalimbali, haya yote yanatokana na upeo mdogo na mifumo dume ambayo unamweka mwanamke katika nafasi ya kuwa chombo cha kuwafurahisha na kuwastarehesha wanaume.

Aghalabu wanawake vijijini hufanywa vyombo vya uzalishaji mali na kuzaa watoto. Ufisadi wa mali za umma unaofanywa na baadhi ya viongozi una mchango mkubwa wa kulifanya taifa letu liendelee kubaki masikini.

Lazima tukubali kuwa, umasikini unatishia amani na ustawi wa nchi yetu na dunia nzima. Umoja wa Mataifa ulisukumwa na kutoa Malengo ya Milenia (MDGs) ambapo umasikini unapaswa kushughulikiwa kwa nguvu zote ili mwaka 2015 angalau upungue na kuifanya dunia kuwa mahali pema pa kufaa binaadamu kuishi.

Sasa ni 2018, je tumefanikiwa? Nani wa kumlaumu? Fikra zetu ama serikali inayoongozwa na CCM kwa kutokuwa na mikakati chanya na endelevu?.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & Uchambuzi

Vijana wanavyoandaliwa kuziba pengo la ujuzi sekta ya madini

Spread the loveMOJAWAPO ya sekta ambazo katika miaka ya 2000 hazikuwa na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Lowassa: Mwanasiasa aliyetikisa CCM, Chadema

Spread the loveWAZIRI Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki Dunia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

error: Content is protected !!