Tuesday , 30 May 2023
Home Habari Mchanganyiko Watano wahukumiwa kunyongwa kesi ya Bilionea Msuya
Habari Mchanganyiko

Watano wahukumiwa kunyongwa kesi ya Bilionea Msuya

Kitanzi
Spread the love

WATU watano wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Moshi kuwakuta na hatia ya kumuuwa kwa kukusudia Mfanyabiashara wa Madini Arusha Bilionea Erasto Msuya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Moshi … (endelea).

Leo Mbele Jaji Jaji Salma Maghimbi ametoa hukumu kwa washitakiwa hao watano na kumwachia huru mshitakiwa namba mbili Shwaibu Jumanne baada Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka yake.

Washtakiwa watano walio hukumiwa adhabu hiyo ni pamoja na Sharifu Mohamed mshitakiwa namba moja, Mussa Mangu mshitakiwa namba tatu, Karim Kuhundwa mshitakiwa namba tano, Sadick Mohamed mshitakiwa namba sita na Ally Mussa Majeshi mshitakiwa namba saba.

Jaji Maghimbi alisikiliza mashahidi 32 wa upande wa jamhuri na vielelezo 26 vya ushahidi wa kesi hiyo ambapo upande utetezi washtakiwa walijitetea wenyewe.

Ushahidi wa Jamhuri wenye vielelezo 26 ndio uliowatia hatiana washtakiwa hao watano ambapo vilionyesha kuwa tarehe 7 Agosti mwaka 2013 eneo la Mijohoroni wilayani Hai Bilionea Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi na bunduki ya kivita ya Sub Machine Gun (SMG).

Katika eneo la tukio, kuliokotwa maganda ya risasi za SMG 22 huku gari ya marehemu aina ya Range Rover T800 CKF, bastola zake na simu zake mbili zikikutwa eneo la tukio.

Jaji Salma Maghimbi aliyesikiliza kesi hiyo, ilipokea vielelezo kadhaa vya kesi hiyo ikiwamo bunduki ya SMG na maganda 25 ya risasi.

Pia, ilipokea pikipiki mbili, moja aina King Lion T751 CKB na Toyo 316 CLG zinazodaiwa na mashahidi wa upande wa mashtaka, kuwa zilitumika kusafirisha wauaji.

Mbali na vielelezo hivyo, Mahakama ilipokea vielelezo vya nyaraka ambavyo ni maelezo ya onyo ya kukiri kosa ya washtakiwa watatu na maelezo ya ungamo yaliyotolewa kwa mlinzi wa amani.

Maelezo hayo ya onyo ni ya mshtakiwa wa kwanza, Sharifu Mohamed, mshtakiwa wa tatu, Mussa Mangu, mshtakiwa wa saba, Ally Majeshi na maelezo ya ungamo ni ya mshtakiwa Karim Kihundwa.

Pia, Mahakama ilipokea maelezo ya mashahidi watano wa upande wa mashtaka na kuyasoma mahakamani baada ya jitihada za upande wa mashtaka kuwapata kugonga mwamba.

Mshitakiwa namba nne aliachiwa huru tarehe 14 Mei mwaka huu baada ya mahakama kumkutaka hana mashtaka ya kujibu ambapo Mfanyabiashara Mwakipesile alikuwa miongoni mwa washtakiwa lakini mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa kutumia mamlakaka yake, alimfutia shtaka hilo Aprili 17,2014.

Hata hivyo jaji Maghimbi alisema wakati washtakiwa wanafunguliwa mashtaka mwaka 2013, walikuwapo nane, lakini kuna mshtakiwa mmoja ambaye hata hivyo hakumtaja kwa jina aliachwa njiani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wenye ulemavu waiomba MISA-TAN iwajengee uwezo wa uhuru wa kujieleza

Spread the love  TAASISI ya vyombo vya Habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wajawazito 2000 Korogwe washiriki Marathon, Mwenyekiti UWT amsifu Jokate

Spread the loveWANAWAKE wajawazito zaidi ya 2000 wilayani Korogwe mkoani Tanga wameshiriki...

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

error: Content is protected !!