Wednesday , 27 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani: China ni tishio
Kimataifa

Marekani: China ni tishio

Donald Trump
Spread the love

MAREKANI inapiga yowe kwamba, China inanyemelea nafasi yake ya kuwa taifa kubwa duniani. Inasema China inaendesha ‘vita baridi,’ pia ni tishio. Anaripoti  Yusuph Katimba…(endelea).

Akiwa kwenye semina ya masuala ya Jukwa la Ulinzi ya Aspen (Aspen Security Forum) wakati wa kipengele cha kujadili ukuaji wa China mwishoni mwa wiki, Michael Collins wa Shirika la Kijasusi la Marekani la CIA alielekeza mashambulizi yake kwa taifa hilo la Asia.

Amesema, lengo la operesheni zinazofanywa na China ni kutaka kuchukua nafasi ya Marekani kama taifa linaloongoza kwa nguvu zaidi duniani.

Collins amesema kwamba, Rais wa China Xi Jinping na serikali yake wapo wenye vita baridi dhidi ya Marekani.

Amesema kuwa, vita baridi inayopiganwa na China dhidi ya taifa lake (Marekani) haijawahi kushuhudiwa na ni tofauti na vita baridi ya awali.

“…vita baridi hii si kama ile tuliyowahi kuishuhudia wakati wa vita vya baridi,” amesema Collins na kuongeza kuwa China inatumia kila aina ya mamlaka iliyonayo iwe halali au haramu, iwe ya umma au ya kibinafsi na ya kiuchumi ama ya kijeshi ili kudhoofisha msimamo wa mpinzani wake.

“Mwisho wa siku wanataka kila nchi kote ulimwenguni, wakati wa kuamua maslahi yake juu ya masuala ya sera, wawe upande wa China na sio Marekani,” amesema.

Maoni ya Collins yamefanana na yale ya maofisa wengine wakuu wa Marekani akiwemo Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la nchi hiyo (FBI), Christopher Wray na Dan Coats ambaye ni Mkurugenzi wa National Intelligence.

“Nadhani China, kwa njia nyingi inawakilisha tishio kubwa zaidi, lenye changamoto kubwa zaidi ambalo tunakabiliwa kama nchi,” amesema Wray.

Wote hao wameieleza kuwa China ni miongoni mwa nchi hatari zaidi kwa taifa la Marekani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

Kimataifa

Uvamizi wa kijeshi Milango ya bahari ya Taiwan G7 yapinga China

Spread the loveMKUTANO wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi za...

error: Content is protected !!