Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto
BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Screenshot
Spread the love

Mafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na mtoto ni moja ya matokeo makubwa ya kuimarika kwa huduma za afya nchini kutokana na uwekezaji wa Serikali pamoja na mchango wa wadau mbalimbali katika jitihada hizo ikiwemo sekta binafsi.  Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, Kanali Wilson Sakulo(watatu kulia) akipiga makofi baada ya kupokea vitanda vya kulalia wagonjwa na kitanda kimoja cha uchunguzi kwa wagonjwa(examination bed) kwa Zahanati ya Luzinga kutoka kwa aliyekuwa Kaimu Meneja wa NMB kanda ya Ziwa Dickson Richard(wa pili kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika wilayani Missenyi mwezi Oktoba mwaka jana.

 Mfano mzuri wa ushiriki wa taasisi binafsi katika jitihada hizo za kitaifa ni Benki ya NMB ambayo ufadhili wake umesaidia sana kulidhibiti kwa kiasi kikubwa tatizo hilo la kiafya katika kanda yake ya ziwa inayojumuisha mikoa minne.

 Kanda hiyo imekuwa ni mnufaika mkubwa wa vifaa tiba na misaada mingine inayotolewa na benki hiyo kuzisaidia hospitali na vituo vya afya katika kuunga mkono azma ya Serikali ya kuboresha ubora na kurahisisha upatikanaji wa matibabu na huduma nyingine mtambuka.

 Viongozi, wanufaika na maafisa wa NMB Kanda ya Ziwa wanasema ushiriki wa NMB umechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za uzazi, mama na mtoto katika mikoa ya kanda hiyo ambayo ni Mara, Kagera, Mwanza na Geita.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mwanangwa iliyopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza, Consolata Simba, akionesha baadhi ya vitanda, Magodoro namashuka waliookea kutoka kw Benki ya NMB ambavyo kwa sasa vinatumika katika wodi ya kupumzikia wazazi.

 Wakizungumza kwa nyakati tofauti hivi karibuni na waandishi wa habari na maafisa wa NMB kutoka makao makuu, walisema vitanda vya kawaida na vya kujifungulia wazazi, magodoro na vifaa tiba vingine inavyovitoa vimekuwa ni uwekezaji wenye tija na afua muhimu katika kusaidia kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na watoto.

 Aidha, ujumbe huo ambao ulikuwa katika ziara ya kutathimini shughuli za uwajibikaji wa NMB kwa jamii (CSR) katika mikoa mitatu ya kanda hiyo, ulifahamishwa pia jinsi wananchi wanavyouthamini mchango huo na unavyosaidia kuboresha mazingira ya kuwahudumia wazazi na watoto.

 Mikoa iliyotembelewa na timu hiyo ya CSR iliyoshuhudia mafanikio makubwa ya ufadhili wa NMB katika kuzitatua changamoto mbalimbali za kijamii zinazowakabili wananchi ni Geita, Mara na Mwanza.

Screenshot

 Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Buzuruga mkoani Mwanza, Dk. William Mtinginya, ufadhili wa NMB si tu umesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo na maradhi, bali pia umesaidia kuongeza idadi ya akina mama na watoto wachanga wanaohudumiwa.

 “Tumeweza kupunguza idadi ya vifo vinavyoweza kuzuilika vya wazazi na vichanga lakini pia wateja wa huduma ya uzazi wameongezeka na sasa wazazi wapya 20 wanahudumiwa hapa kwetu kila mwezi,” Dr Mtinginya aliimbia timu hiyo ilipokitembelea kituo hicho katika Wilaya ya Ilemela.

 “Kabla ya ufadhili wa vifaa kutoka NMB tulikuwa tunawahudumia wajawazito 200 hadi 300 kwa mwezi lakini sasa hivi wamefikia 600 huku idadi ya wanaojifungulia majumbani nayo ikipungua sana,” aliongeza.

Katika Kituo cha Afya Katoro mkoani Geita, Dk. Rhoda Haule aliomba usaidizi zaidi kutoka taasisi nyingine za sekta binafsi akisisitiza umuhimu na uhitaji wake katika kuyanusuru maisha ya wazazi na watoto wachanga.

 Mganga huyo mfawidhi alisema moja ya faida za vitanda vya NMB kwao imekuwa ni kuondokana na changamoto ya akina mama kulala watatu hadi watano kwenye kitanda kimoja wakisubiri kujifungua.

 Aidha, Dk. Haule alisema pamoja na kuboreka kwa huduma kwenye wodi za wazazi ambazo sasa hivi zinawahudumia wajawazito kati ya 750-900 kila mwezi, bado kuna umuhimu wa kufanya maboresho zaidi.

 “Jumla tuna vitanda 102, kwahiyo huduma zetu zitaimarika zaidi endapo tutapata wafadhili wengine kama NMB,” alieleza na kubainisha kuwa moja ya uhitaji wao mkubwa kwa sasa ni kuwa na jengo la kisasa la kufulia.

 Akiipongeza NMB kwa msaada wa vitanda, mashuka na magodoro iliyopata Zahanati ya Mwanangwa inayohudumia wakazi 20,000 wa Kata ya Mabuki na vijiji vya jirani wilayani Misungwi, Mwanza, Dk. Consolata Simba, alisema huduma ya afya ya mama na mtoto ni suala mtambuka katika kuokoa maisha, kuimarisha ustawi wa jamii na kuchochea maendeleo ya taifa kwa ujumla.

 Mganga huyo alisema baadhi ya vifo vya mama na mtoto utokana na umbali wa kuzifikia huduma stahiki pamoja na akina mama kujifungua kienyeji majumbani.

 Changamoto nyingine nyingi katika eneo hili nyeti katika afya ya jamii ni matokeo ya upungufu wa wahudumu wa afya wenye ujuzi wa kutosha, ukosefu wa vifaa tiba vya msingi, kutokuwepo kwa mfumo unaojitosheleza wa rufaa pamoja na huduma duni za dharura za uzazi na watoto wachanga.

 Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa theluthi moja ya vifo vyote vya watoto nchini vinatokana na watoto 390 walio chini ya umri wa miaka mitano kufa kila siku kwa sababu zinazoweza kuzuilika, magonjwa ambayo yanatibika pamoja na uhaba wa vifaa vya kuwahudumia.

 Wataalamu wa afya za watoto wanasema vingi vya vifo hivi utokana na changamoto za afya za akina mama wanapokuwa wajawazito na mazingira duni ya kujifungulia na kuvillelea vichango hali inayoonyesha unyeti wa mchango wa Benki ya NMB katika maendeleo ya sekta ya afya nchini.

 Uwekezaji huo si tu ni wakuigwa bali pia ni wa kuongezwa kama walivyobainisha madaktari wa Kanda ya Ziwa kutokana na faida zake lukuki ikiwemo kuwaboreshea mazingira ya kazi.

 Ikiwa benki kinara wa huduma za kifedha, NMB pia inaongoza kwa uwajibikaji kwa jamii katika Kanda ya Ziwa yenye utajiri mkubwa wa rasilimali na watu wengi kuliko maeneo yote nchini.

 “Sambamba na dhamira yetu ya kurudisha fadhila kwa jamii, tunawekeza vya kutosha katika programu mbalimbali endelevu za kijamii kwa kila mwaka kutenga asilimia moja ya faida baada ya kodi katika shughuli za CSR,” meneja mpya wa NMB Kanda ya Ziwa, Wogofya Mfalamagoha, alisema.

 “Mwaka jana, bajeti hii ilifikia zaidi ya TZS bilioni 6 ili pia kukidhi shughli za uendelevu ambazo zilijumuisha upandaji miti kote nchini kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,” Wogofya aliuwaambia ujumbe wa CSR.

 Ufadhili wa NMB unaozingatia vipaumbele vya taifa vya afya ufanyika kwa kutilia maanani hasa uhaba wa vitanda kama moja ya changamoto kubwa mahospitalini na vituo vingi vya afya.

 Ripoti na nyaraka za benki hiyo zinaonyesha kuwa sehemu ya TZS bilioni 12 ilizoziwekeza kwenye CSR katika kipindi cha miaka 10 kufikia mwaka 2021 zilizisaidia vituo vya afya zaidi ya 600 huku watu zaidi ya 210,100 wakinufaika na kufadhiliwa kwa vituo 42 kati ya mwaka 2020 na 2022.

 NMB pia uchangia vifaa vya ujenzi kama ilivyofanya mkoani Mara mwaka 2022 ilikotoa TZS milioni 30 kusaidia ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika Zahanati ya Busawe wilayani Serengeti.

 Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wake, Dk. Juma Rajabu Ali, wodi hiyo ya kisasa ikikamilika kama ilivyopangwa mwezi Mei mwaka huu itapelekea wajawazito wanne kujifungua kwa wakati mmoja ikilinganishwa na idadi ya akina mama wawili au watatu wanaojifungua kwa siku sasa hivi.

 Aidha, Dk. Juma alisema matokeo mengine chanya ya usaidizi wa NMB ni kusaidia kupunguza vifo vya vichanga ambavyo kwa sasa ni asilimia 12-15 kutokana na hasa umbali wa kuzifikia sehemu ambako huduma stahiki zinapatikana.

 “Kupatikana ufadhili huu kwa wakati kusaidia kuukamilisha mradi huu wa ujenzi kumewagusa viongozi na wananchi kwa sababu ya umuhimu wake katika maisha ya wananchi wa hapa,” mjumbe wa utekelezaji mradi, Alexandar Faustin Machugu, alimwambia mwandishi wa habari hii.

 Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Busawe, Suto Richard, alisema jambo ililolifanya Benki ya NMB liliwafurahisha watu na kuwahamasisha kujitolea kwa hali na mali kuchangia ujenzi huo wengi wakisomba mchanga na mawe pamoja na kufanya kazi nyingine zilizo ndani ya uwezo wao.

“Tunaishukuru sana NMB kwa kutusaidia kwa sababu siku si nyingi akina mama wajawazito katika eneo hili na vijiji vya jirani hawatalazimika tena kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma ya kujifungua, hilo litakuwa linafanyika hapa” mmoja wa wanakijiji wa Busawe, Bi Robina Mahemba Machota, alisema.

Akizungumzia CSR ya NMB kwa ujumla, Meneja wa Tawi la NMB la Mugumu, Bw John Nyoni, alisema wanashirikiana kwa karibu na mamlaka pamoja na viongozi kutatua changamoto zinazozikabili jamii kwa kuzingatia dhamira ya benki hiyo ya kuwa chachu ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cheza sloti ya Zombie Apocalypse na ushinde kirahisi

Spread the love Wengi wetu hupenda filamu za Mazombie huwa zinatishakidogo lakini...

Biashara

Ushirikishwaji wa wafanyakazi ni muhimu katika utekelezaji wa sera za afya na usalama kazini

Spread the love  KILA ifikapo Aprili 28 ya kila mwaka, dunia huadhimisha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Biashara

Wazir Jr kinara wa ufungaji KMC FC ajiunga Meridianbet

Spread the love    MUITE Wazir Jr ‘The King of CCM Kirumba’,...

error: Content is protected !!