Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Tanzania yaweka rekodi mauzo ya madini
Biashara

Tanzania yaweka rekodi mauzo ya madini

Spread the love

WAZIRI wa Madini, Dk. Doto Biteko amesema sekta ya madini imevunja rekodi katika mauzo yake kwenye masoko mbalimbali, ambayo yamekua hadi kufikia thamani ya Sh. 8.3 trilioni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Dk. Biteko ameyasema hayo leo tarehe 10 Machi, 2022 jijini Dodoma wakati akielezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Katika kipindi hiki cha uongozi wa Serikali ya sita, sekta ya madini imeweka rekodi ya juu kabisa ya mauzo ya moja kwa moja ya madini tofauti, yenye thamani ya Sh. 8.3 trilioni, yameuzwa kwenye masoko mbalimbali,”amesema Dk. Biteko.

Waziri huyo wa madini amesema, kutokana na kukua kwa mauzo hayo, wizara yake imekusanya tozo mbalimbali ikiwemo ya mrabaha, zenye thamani ya Sh. 597.5 bilioni.

Dk. Biteko amesema, mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa umekuwa hadi kufikia asilimia 7.3, kutoka asilimia 6.5 kabla ya Serikali hiyo kuingia madini.

“Chini ya uongozi wa Rais Samia, mchango wa sekta katika pato la Taifa umeendelea kuongezeka kwa kasi kuliko kipindi chochote, katika robo moja ya mwaka hadi mwingine umeongezeka, mfano hadi Septemba 2021 umekuwa kufikia asilimia 7.3 kutoka asilimia 6.5 iliyokuwepo kabla,” amesema Dk. Biteko.

Amesema, katika mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia, migodi mitatu ya madini, imelipakodi ya dola za Marekani 652 milioni (Sh. 1.5 trilioni), ambapo Kampuni ya Madini ya Twiga imelipa dola za Marekani 304 milioni. Geita Gold Mining (dola za Marekani 268 milioni) na Williamson Diamond Limited-WDL ( dola za Marekani 80 milioni).

Dk. Biteko amesema ushiriki wa Watanzania katika shughuli za madini umeongezeka kutoka asilimia 48 hadi 63, huku thamani ya biashara zao zikiongezeka kufikia Sh. 1.33 trilioni.

Wakati huo huo, Biteko amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani, Serikali yake imeendelea kudhibiti utoroshwaji madini, kwa kuweka mikakati mbalimbali, ikiwemo ya kuondoa urasimu kwenye utoaji vibali.

“Vitendo hivyo sitaki kusema vimeisha, ila bila shaka yoyote naweza kusema vimepungua kwa kiasi kikubwa na waliopunguza ni wachimbaji wenyewe hawaoni sababu ya kutorosha madini kupeleka nje ya nchi bila kuyalipia kodi,” amesema Biteko.

1 Comment

  • Moja, mbona hakuna Barrick Gold au African Barrick Gold, si wameunda Katanga?
    Naomba serikali ianzishe kampuni na siyo wageni.
    Pili, vile vichwa 300 bungeni vitunge sheria kwamba hakuna kampuni ya nje itaruhusiwa kuingia ubia na kampuni nyingine yeyote bila uchunguzi wa wazi. Ule mchezo mchafu wa makanikia usirudiwe tena.
    Kwa nini Williamson Diamonds ina pato dogo hivyo?
    Tatu, uchimbaji wa mashimo ya wazi (open pits) usiendelee kupewa wawekezaji wa nje. Serikali iunde kampuni, iwekwe kwenye hisa watanzania wanunue hisa na mtaji utapatikana. Tuachane na utegemezi.
    Nne, leseni za kuhodhi madini zifutwe. Helium One ni mfano. Hawa ndiyo Tananite One tuliyoifungia. Tunajua wamekuja wawekezaji hewa na kuhodhi maeneo ili wayauze.
    Mwisho, tuache kutumia “usajili wa nje” kuhalalisha kampuni hizo. Nyingi ni haramu lakini zimekwenda nchi marafiki na kujisajili huko halafu zinakuja kwetu. Usalama wa Taifa sasa ianze kufanya kazi ya usalama wa uchumi kama wajapani na wakorea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!