ALIYEKUWA mtia ya kugombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Maryrose Majinge amewataka Watanzania kujifunza kuyatazama mambo mema kwa na kuacha dhana na fikra hasi kwa watu au viongozi. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).
Akizungumzia mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, Dk. Majinge ambaye pia ni Mwanaharakati wa maendeleo ya watu, wakati anakabidhiwa madarakani watu walidhani asingeyamudu lakini sasa amedhihirisha kuwa wanawake wanaweza.
Amesema watu waliokuwa wanamtazamo juu kuwa Rais Samia hataweza fikra zao hasi hazina muafaka mwema kwa Taifa.
Ameeleza mwaka mmoja wa Rais Samia umetoa taswira chanya Taifa hivyo Watanzania wanapaswa wamuunge mkono kindakindaki katika uongozi wake.
Aidha, Dk. Majinge amependekeza Sheria ya Mvuto kutumika vizuri ili kuondosha tabia ya kudhaniana mambo yasiyopendeza au tabia ya kuamini mtu fulani hawezi.
Ameitaja Sheria ya mvuto kuwa inakusudia watu wawaze mambo mazuri.
Ameeleza kuwa sheria hiyo ya mvuto ikitumiwa sambamba na kanuni ya dhahabu watu wataondokana na fikra hasi kutilia mashaka kuogopana.
Pia amesema kuwa kanuni ya kuwa na matumani yaani watu kutokataa tamaa itaboresha fikra za watu.
Leave a comment