Saturday , 11 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Tahadhari homa ya uti wa mgongo
Afya

Tahadhari homa ya uti wa mgongo

Spread the love

 

SERIKALI imewataka Watanzania kuchukua tahadhari kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo uliotokea katika jimbo la Tshopo nchini DRC Congo. Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARCo … (endelea).

Taarifa iliyotolewa jana tarehe 16 Septemba, 2021 na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Aifelo Sichwale, imesema vimelea vya ugonjwa huo huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa au kukaa na mtu mwenye maambukizi.

Aidha, taarifa zilizotolewa Septemba 8, 2021 na Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, mlipuko huo unaoambukiza ni tishio kwa sasa Barani Afrika.

Hata hivyo, Dk. Sichwala amesema ni vyema kuendelea kuchukua tahadhari kwani magonjwa hayana mipaka, hususani mikoa inayopakana na DRC.

“Ugonjwa huo wa mlipuko husababishwa na bakteria wanaojulikana kama ‘Neisseria meningitides’. Ugonjwa huu huchukua siku mbili hadi 10 tangu kuambukizwa hadi kuanza kuonyesha dalili,” amesema Dk. Sichwale.

Akizungumzia dalili za ugonjwa huo, Dk Sichwale amesema ni homa kali, kichwa kuuma, kutapika, kuogopa mwanga, kuchanganyikiwa na shingo kukakamaa.

“Ugonjwa huo unaweza sababisha madhara makubwa kwenye ubongo, kupotea kwa usikivu au ulemavu mwingine wa kudumu na hata kupoteza maisha.

“Ili kuzuia maambukizi wananchi wanapaswa kuepuka mikusanyiko ya watu wengi hasa wakati wa milipuko, makazi yazingatie mzunguko mzuri wa hewa. Hivyo wananchi wanashauriwa kutoa taarifa mapema endapo wataona mtu yeyote mwenye dalili zilizotajwa ili hatua stahiki za kudhibiti zichukuliwe mapema,” amesema.

Dk. Sichwale ameagiza mikoa yote inayopakana na DRC ikiwemo Kigoma, Rukwa, Kagera, Katavi na Songwe kuchukua hatua mbalimbali za tahadhari ikiwemo kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa ugonjwa huo na utoaji taarifa kupitia mfumo wa utoaji taarifa za magonjwa ya mlipuko.

Ameitaka mikoa hiyo kuongeza nguvu ya ufuatiliaji katika mipaka, hususani kwa wageni wanaoingia nchini kutoka DRC.

“Naagiza kuimarisha ufuatiliaji wa wagonjwa katika ngazi ya jamii hususani maeneo ya mipakani ili kutambua mapema mgonjwa na kuwaandaa watoa huduma na vituo vya huduma kukabiliana na ugonjwa huu endapo utajitokeza,” amesema.

Aidha, amesema Wizara inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa ugonjwa huo nchini DRC na kuchukua hatua ili kuzuia na kujiandaa kukabiliana na tishio la ugonjwa huo endapo utajitokeza nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!