SPIKA wa Bunge la Marekani, Kevin McCarthy, ameondolewa madarakani kwa tuhuma za kukiasi chama chake cha Republican, akituhumiwa kushirikiana na Serikali ya Rais Joe Biden, anayetoka chama cha Demcratic. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
MacCarthy ameng’olewa madarakani jana Jumanne, baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, na wabunge wenzake wa Republican, ambao wanaongoza kwa kuwa na idadi kubwa na nguvu bungeni.
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Swahili, kura hiyo ilitokana na hoja ya kutokuwa na imani na MacCARTHY, iliyowasilishwa na mbunge wa Republican, Matt Gaetz, katika mhimili huo Jumatatu iliyopita.
Miongoni mwa sababu za hoja ya Gaetz, ni madai ya McCarthy kufanya makubaliano ya siri na Ikulu ya White House, kuendelea kuifadhili Ukraine, tuhuma ambazo mwanasiasa huyo amezikanusha.
Leave a comment