Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara Vodacom M-Pesa yajumuika kusherehekea siku ya urithi wa watu wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania
Biashara

Vodacom M-Pesa yajumuika kusherehekea siku ya urithi wa watu wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania

Spread the love


KATIKA jitihada za kukuza na kuendeleza umoja miongoni mwa Watanzania na watu kutoka mataifa mengine, Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya M-Pesa iliungana na raia wa Afrika ya Kusini kusherehekea siku ya urithi wa taifa hilo jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Siku ya urithi wa Afrika ya Kusini ni sikukuu ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 24 kwa madhumuni ya kusherehekea utamaduni na utofauti wao katika nyanja kiimani na kimilia.

Akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika ofisi za ubalozi mwishoni mwa wiki, Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania, Noluthando Mayende-Malepe amewapongeza wananchi wa Afrika ya Kusini wanaoishi hapa kwa kujitokeza kusherehekea siku hii muhimu kwao.

“Ikiwa tunatimiza miaka 29 tangu kupata uhuru kwa taifa letu na tunatarajia mwakani itakuwa ni miaka 30, hatuna budi kujivunia kwa mshikamano tunaendelea kuunyosha. Siku ya leo hapa tunasherehekea pamoja na mataifa kama vile Comoro, Namibia, Msumbiji, na Somalia ambao mabalozi wao wote wako hapa. Hii ni ishara nzuri kwa bara letu la Afrika ambalo watu wake wana historia ndefu tangu kipindi cha harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni na mpaka sasa tuko huru. Ninajivunia kuona mataifa yetu yanashirikiana katika shughuli tofauti za kiuchumi na kijamii, lakini kikubwa zaidi ni kuona amani na upendo vinaendelea licha ya changamoto mbalimbali tunazopitia. Ni matumaini yangu mwakani tutajumuika pamoja pia ambapo tutakuwa tunasherehekea miaka 30 ya uhuru wetu,” alimalizia Mayende-Malepe.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa M-Pesa, Bw. Epimack Mbeteni amebainisha kuwa ni heshima ya kipekee kuwa sehemu ya sherehe hizi ambazo zina maana kubwa kwa watu wa taifa la Afrika ya Kusini ukizingatia kwamba zinasaidia kurithisha mila na tamaduni ambazo zimerithishwa na vizazi tofauti muhimu kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na kijacho.

“Uwepo wa ushirikiano imara na wa kudumu kati ya Afrika ya Kusini na nchi nyingine umekuwa na manufaa makubwa pia hata kwetu sisi watoa huduma. Kwa miaka mingi tumekuwa tukishuhudia raia wa pande zote mbili wamekuwa huru kuwekeza na kufanya kazi bila ya kupata changamoto zozote,” alisema Mbeteni.

Mataifa ya Afrika ya Kusini na Tanzania yamekuwa na historia ndefu kwa muda mrefu kutokana na ushirikiano wao tangu enzi za kutafuta uhuru mpaka sasa ambapo yanashirikiana kwa shughuli mbalimbali za kichumi na kijamii. Hivi sasa, tunajionea makampuni mbalimbali baina ya nchi hizi mbili yakija kuwekeza huku wananchi wake wakiweza kufanya kazi bila ya vikwazo vyovyote.

“Uwepo wa ushirikiano imara na wa kudumu kati ya Afrika ya Kusini umekuwa na manufaa makubwa pia hata kwetu sisi watoa huduma. Kwa miaka mingi tumekuwa tukishuhudia raia wa pande zote mbili wamekuwa huru kuwekeza na kufanya kazi bila ya kupata changamoto zozote.

”Dunia inashuhudia maendeleo ya kidigitali yanayochochewa na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano. Hii inapelekea watu kufanya kazi sehemu tofauti duniani bila ya hofu ya usalama wao na uhakika wa kuwasiliana na familia walizoziacha nyuma,” aliongezea Mkurugenzi wa M-Pesa.

Kwa kulitambua hilo Vodacom kupitia huduma yake ya M-Pesa imekuwa ikifanya maboresho ya mara kwa mara ili kuwawezesha wateja na Watanzania kwa ujumla kuendelea na shughuli zao bila ya kikwazo cha kuwa katika ardhi ya nchi nyingine.

Mnamo 2014, ilizindua huduma ya kutuma na kupokea pesa kwa mara ya kwanza ambapo wateja waliweza kuitumia baina ya nchi za Kenya na Tanzania pekee, lakini kwa sasa wanaweza kufanya hivyo kwa takribani nchi 8 za SADC ikiwemo wakiwa Afrika ya Kusini

“Hivi karibuni tumezindua laini ya kielektroniki au eSim ambayo huchapishwa moja kwa moja katika simu hivyo kurahisisha mtu akisafiri kwenda nchi nyingine kubadili wasifu wake kwa urahisi na kuendelea kuwasiliana bila ya usumbufu wa kusajili laini nyingine. Huduma hii inaimarishwa zaidi na upatikanaji wa vifurushi vya intaneti/data vya kimataifa hivyo unaendelea na shughuli zako bila ya wasiwasi pamoja mtandao wenye kasi na ufanisi wa 5G uliozinduliwa Oktoba 2022, kwa matumizi binafsi na wafanyabiashara,” alimalizia Mkurugenzi wa M-Pesa.

Kwa sasa kuna huduma nyingine lukuki ambazo zinapatikana ndani ya applikesheni ya M-Pesa Super App ambayo inazidi kuwezeshwa kuwa na applikesheni za huduma tofauti ikiwemo ya kukata tiketi za ndege. Lengo ni iwe inajitosheleza mtu kufanya manunuzi na malipo ya bidhaa tofauti sehemu moja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cheza sloti ya Zombie Apocalypse na ushinde kirahisi

Spread the love Wengi wetu hupenda filamu za Mazombie huwa zinatishakidogo lakini...

Biashara

Ushirikishwaji wa wafanyakazi ni muhimu katika utekelezaji wa sera za afya na usalama kazini

Spread the love  KILA ifikapo Aprili 28 ya kila mwaka, dunia huadhimisha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Biashara

Wazir Jr kinara wa ufungaji KMC FC ajiunga Meridianbet

Spread the love    MUITE Wazir Jr ‘The King of CCM Kirumba’,...

error: Content is protected !!