UONGOZI wa klabu ya Simba umetoa pole kwa wapinzani wao Yanga kufuatia ajali ya gari la mashabiki wa timu hiyo lililokuwa linaelekea katika mchezo wao wa leo dhidi ya Coastal Union, jijini Arusha. Anaripoti Urumasalu Kisung’uda, TUDARCo … (endelea).
Ajali hiyo iliyosababisha kifo cha mshabiki mmoja na majeruhi watano ilitokea jana usiku tarehe 19 Agosti, 2022 katika barabara ya Bagamoyo eneo la Mwetemo.
Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Simba imetoa pole kwa ndugu wa marehemu pamoja na kuwaombea mashabiki waliopata majeraha katika ajali hiyo.
https://twitter.com/SimbaSCTanzania/status/1560936973602283521/photo/1
Majeruhi watano wa ajali hiyo, wawili wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata ilhali wengine watatu wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo baada ya kupata majeraha madogo madogo.
Chanzo cha ajali hiyo ni gari iliyokuwa imebeba mashabiki wa Yanga kutaka kulipita gari lingine lililokuwa mbele yake (overtake) na kukutana na gari hilo la mzigo aina ya Canter ambalo katika harakati za kukwepa kugongana uso kwa uso likaipiga ubavuni (pasi) basi hilo aina ya Coaster.
Leave a comment