October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Juliana Cherera; kigogo tume ya uchaguzi anayetia mchanga ushindi wa Ruto

Spread the love

Jina la Juliana Cherera ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka kutoka nchini Kenya (IEBC), limepata umaarufu mkubwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa taifa hilo la Afrika mashariki. Cherera aliongoza jopo la makamishna wanne kupinga matokeo yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Wafula Chebukati.

Tarehe 15 Agosti, Chebukati alimtangaza Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi huo uliofanyika tarehe 9 Agosti, 2022 na kumbwaga mshindani wake wa karibu, Raila Odinga.

Aidha, katika tume hiyo iliyo na makamishna saba, wanne walijiengua na kujiweka kando na matoke ohayo wakiongozwa na Cherera ambaye alitoa sababu za kukataa matoke ohayo kuwa ni pamoja na kukosewa kwa hesabu pamoja na Chebukati kujipa madaraka ya kutangaza bila kuafikiana na makamishna wenzie wa tume hiyo.

Wanne hao Irene Cherop, Justus Abonyo, Francis Wanderi na Juliana Cherera, walipinga matokeo ya uchaguzi huo katika nafasi ya rais.

Tangu wakati huo, Wakenya wameibua maswali mengi na mojawapo ambalo linavutia wengi ni kutaka kumfahamu mwanamke aliyesimama bila uoga kupaza sauti yake.

Juliana Whonge Cherera ni nani?

Juliana Whonge Cherera ndiye Makamu mwenyekiti wa IEBC kwa sasa ambaye aliapishwa na Jaji Mkuu Martha Koome katika Mahakama ya juu zaidi jijini Nairobi mnamo Septemba 14, 2022.

Mbali nay eye, pia  Irene Cherop, Justus Abonyo, Francis Wanderi waliapishwa na kujaza nafasi zilizoachwa wazi baada ya kujiuzulu kwa Roselyn Akombe,  Margaret Mwachanya, Paul Kurgat na Connie Maina walioondoka baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2017.

Jukumu la Cherera na  Chebutaki ni kuhakikisha Makamishna wanawezeshwa kutekeleza majukumu yao wakati wote.

Elimu

Cherera, ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Elimu, Uongozi na Usimamizi wa Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Methodist cha Kenya (KEMU) pia ana Shahada ya Elimu  (Sanaa) kutoka Chuo kikuu  cha Kenyatta akibobea katika Jiografia na Kiswahili.

Kazi;

Cherera, alianza kazi yake ya ualimu ambayo sasa anajivunia uzoefu wa zaidi ya miaka 18 katika sekta ya Elimu  na Usimamizi ambapo hapo awali alifanya kazi kama Afisa Mwandamizi (CO) katika kaunti ya Mombasa katika Kitengo mipango na maendeleo.

Aidha, Cherera, alikuwa muongani mwa viongozi ambao, pamoja na wahisani mbalimbali, waliongoza na kuratibu mpango  wa usambazaji wa chakula uliofahamika kama ‘’Pamoja Kwa Mombasa’’.

Mbali na kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya kuratibu miradi ya kusaidia Kaya na kusaidia lishe katika Kaunti ya Mombasa, Cherera, pia ni Katibu wa Mpango wa Kufufua Uchumi na Mikakati ya Kaunti ya Mombasa.

Kwa mujibu wa wasifu wake, Cherera, Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu ya Mpiga Kura, Ubia na Wadau. Makala hii imeandaliwa Felista Mwaipeta TURADCo.

error: Content is protected !!