Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Sheria mpya za habari zawaibua EALS kuwaandaa waandishi kuzikabili
Habari Mchanganyiko

Sheria mpya za habari zawaibua EALS kuwaandaa waandishi kuzikabili

Spread the love

CHAMA cha Wanasheria Afrika Masharika (EALS) kimetoa wito kwa waandishi wa habari kusoma na kuzielewa sheria zinazoongoza sekta hiyo ili kuamka na kupaza sauti kuhusu umuhimu wa marekebisho ya sheria hizo ambazo zimekuwa kikwazo katika utekelezaji wa majukumu yao. Anaripoti Faki Sosi (endelea).

EALS imetoa wito huo juzi Alhamisi katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwanoa waandishi kuhusu mabadiliko ya sheria hizo pamoja na maendeleo ya teknolojia ambayo yametajwa kuipa wakati mgumu sekta ya habari duniani.

Mtendaji Mkuu wa EALS, David Sigano akisisitiza jambo katika mafunzo hayo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyoshirikisha wadau mbalimbali wa sheria, Mtendaji Mkuu wa EALS, David Sigano alisema asilimia kubwa ya waandishi wa habari hawafahamu haki zao ndio maana wamekuwa wakikandamizwa na waajiri na hata pia katika sheria zinazowaongoza kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Alitaja baadhi ya sheria hizo kuwa sheria huduma za habari za mwaka 2016 iliyofanyiwa marekebisho mwaka huu 2023, Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta EPOCA) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022, Sheria ya makosa ya mtandaoni, sheria ya takwimu na sheria nyingine ikiwamo ya sheria ya kazi ambayo waandishi wameshindwa kuitumia kudai haki zao kwa waajiri.

Mshauri mwelekezi wa masuala ya kidijitali kutoka Shirika la Oxfam, Bill Marwa akitoa mada kuhusu mafunzo hayo.

Akifafanua kwa kina kuhusu sheria hizo, Wakili Fulgence Massawe kutoka Kituo cha Sheria Haki za Binadamu (LHRC) aliwatahadharisha waandishi wa habari kuchunga mipaka yao ya kisheria ili wasiingie kwenye mtego wa sheria hizo ambazo bado serikali imegoma kuzifanyia marekebisho licha ya kuwepo kwa vifungu vinavyokwaza uhuru wa habari.

“Mnatakiwa kujifunza namna ya kuogelea kwenye bahari yenye papa bila kumezwa.. kwa sababu katika uongozi wa awamu ya tano, tulipokea kesi nyingi za waandishi wa habari ambao kwa bahati mbaya walitelekezwa na waajiri wao baada ya kupatwa na swahibu na hii yote ni kwa sababu hawakuwa na mikataba ya kazi,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo akitoa mada kwenye mafunzo hayo.

Alisema asilimia kubwa ya waandishi waliotetewa na kituo hicho hawakuwa na mikataba na waajiri wao, jambo ambalo liliwawia vigumu pindi walipobanwa na sheria zinazoongoza sekta hiyo ya habari.

Alitoa mfano katika sheria ya huduma za vyombo vya habari ya 2016, kifungu cha 7 (2), (3) vyote vinatoa maelekezo kwa mamlaka kwamba ni habari gani itangazwe au ichapishwe.

Amesema vifungu hivyo vinaukwaza uhuru wa habari na kwamba mamlaka inakuwa na uhuru zaidi juu ya nini kiwafikie wananchi.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo aliwashauri waandishi wa habari kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia kwa kupambania fursa zinazojitokeza kwenye maendeleo hayo ya kidijitali.

Mbali na kuwaeleza madhila yaliyomkumba katika uongozi wa Rais Jakaya Kikwete na Rais John Magufuli, alisisitiza kuwa mabadiliko ya kiteknolojia ni kama mafuriko, hayawezi kuzuilika hivyo kila mmoja anatakiwa kuenenda nayo.

“Hatutakiwi kukaa pembeni na kuanza kulalamika kuwa mabadiliko haya ya kidijitali yametuletea njaa, magazeti yanakufa… lazima utumie mitandao hii ya kijamii kupata fursa mbalimbali.

“Mathalani hapa Tanzania kwa mujibu wa takwimu za Julai za TCRA watumiaji wa intaneti wamefikia milioni 34, ilihali takwimu za NBS zinaonesha zaidi ya nusu ya Watanzania ni vijana ambao ndio watumiaji wa mitandao hii, sasa jiulize unaitumia vipi hii kama fursa ya kwako kujiingiza kipato?

“Hivyo kila mtandao wa kijamii unapoingia wewe kama mwandishi wa habari na kijana unatakiwa kujiunga lakini pia uutumie kwa faida na sio kuendekeza masuala yasiyo na tija,” alisema.

Hoja hiyo iliungwa mkono na Mshauri mwelekezi wa masuala ya kidijitali kutoka Shirika la Oxfam, Bill Marwa ambaye aliwaonya waandishi wa habari kuwa makini na matumizi ya intaneti na programu zake.

Alitoa mfano kuhusu matumizi ya wifi za bure kuwa zimekuwa zikikusanya taarifa za mtumiaji bila yeye kutambua.

“Baadhi ya wifi hizi za ofa ni hatari sana, kwa sababu yule anayesimamia mfumo huo anaweza kuingia kwenye simu yako na kuchukua kitu chochote ikiwamo hata picha au video za utupu kama ulijipa na kukufanyia chochote kibaya, kwa hiyo unatakiwa kuwa makini sana na hizi data za bure,” alisema.

Alisema upo umuhimu kwa waandishi wa habari kulinda taarifa zao kwa sababu baadhi ya programu za bure hulazimisha mtumiaji kukubali vigezo na masharti jambo wengi hutia tiki (kukubali) bila kuyasoma na mwisho wa siku taarifa za mtumiji huweza kudukuliwa bila kikwazo chochote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!