Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa 500 kujadili ripoti ya kikosi kazi, demokrasia, hali ya siasa
Habari za SiasaTangulizi

500 kujadili ripoti ya kikosi kazi, demokrasia, hali ya siasa

Spread the love

ZAIDI ya watu 500 kutoka taasisi za kisiasa, dini, asasi za kiraia na wengine watakutana kwa siku tatu jijini Dar es Salaam kupokea ripoti ya kikosi kazi na kufanya tathmini ya demokrasia na hali ya kisiasa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yamesemwa na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ali Ahmed wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi jijini Dar e Salaam, huku akiweka bayana kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ndiye atafungua kikao hicho.

Amesema kikao hicho cha aina yake kitafanya tathmini ya utekelezaji wa ripoti ya kikosi kazi, demokrasia na hali ya siasa
“Jumatatu Septemba 11 hadi 13, 2023 wadau wa vyama vya siasa, asasi za kidini, kiraia na wengine watajadiliana kuhusu tathmini ya utekelezaji wa ripoti ya kikosi kazi, demokrasia na hali ya kisasa, tunawaomba watu wote walioalikwa kujitokeza kwa wingi,” amesema.

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ali Ahmed

Ahmed amesema Rais Samia amekuwa akisisitiza 4R katika uongozi wake akimaanisha maridhiano, ustahimilivu, mabadiliko na kujenga upya, hivyo kupitia mkutano huo wadau watapata nafasi ya kujadiliana kwa kina na uhuru.

Naibu Msajili amesema mkutano huo ambao unatarajiwa kufungwa Septemba 13 na Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi umebeba kauli mbiu inayosema imarisha demokrasia dumisha amani, hivyo ni imani yetu kubwa washiriki watazingatia hilo katika mijadala yao.

Amesema mkutano huo unatarajiwa kutoka na maazimio kuhusu utekelezaji wa ripoti ya kikosi kazi iwapo wataona utekelezaji haukufanyika.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Maandalizi amesema mkutano huo ni mwendelezo wa ule wa tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 ambao ulifanyika mkoani Dodoma na kuzaa kikosi kazi ambacho kilipokea maoni ya wadau, ikiwemo mchakato wa kupatika kwa Katiba mpya.

“Waswahili wanasema mwiba ulipoingilia ndipo unapotokea, hivyo tumewaita wadau ili wapate fursa ya kujadili kwa kina kuhusu mapendekezo yao,” amesema.

Ripoti ya Kikosi Kazi
Ripoti ya kikosi kazi ilitoa mapendekezo 19 ya kufanyiwa kazi ambapo moja wapo ni kuhusu mikutano ya hadadhara kuruhusiwa jambo ambalo Rais Samia aliridhia na vyama vya siasa vimeanza kutekeleza kwa vitendo.

Pia Kikosi Kazi kimependekeza Sheria ya Vyama vya Siasa ifanyiwe marekebisho ili, kulipatia Baraza la Vyama vya Siasa mamlaka ya kuishughulikia suala la uvunjifu wa maadili ya Vyama vya Siasa kupitia Kamati yake ya Maadili na Msajili wa Vyama vya Siasa awe na mamlaka ya kuandaa mwongozo wa uchaguzi wa ndani ya vyama.

“Kuweka masharti kwamba idadi ya jinsi moja katika vyombo vya maamuzi vya chama cha siasa isipungue asilimia 40; na kukitaka kila chama cha siasa kuwa na sera ya ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika shughuli za chama husika,” ilisema.

Eneo lingine ambalo Kikosi Kazi kimependekeza ni kuhusu ruzuku kwa vyama vya siasa ambapo mfumo wa sasa wa kugawa ruzuku ya Serikali kwa vyama uendelee, isipokuwa asilimia 10 ya fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa zilizotengwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha husika, igawiwe sawa kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili kwa mujibu wa vigezo na masharti husika.

Pia Kikosi Kazi kimependekeza mfumo wa uchaguzi, kwa Mfumo Mseto wa Uchaguzi uendelee kutumika kwa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Aidha, katika uchaguzi wa Rais ili mgombea ashinde uchaguzi iwe ni lazima apate zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote halali zilizopigwa na uchaguzi wa wabunge, madiwani na uchaguzi wa Serikali za Mitaa uendelee kutumia Mfumo wa Mshindi kwa Kura Nyingi; na Mfumo wa Uwiano wa kura uendelee kutumika kupata wabunge na madiwani wa viti maalum vya wanawake.

“Eneo la nne ni Uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi, Matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa Tanzania kutohojiwa Mahakamani, Watendaji wa Tume ya Uchaguzi, Bajeti ya Tume ya Uchaguzi, Usimamizi wa Uchaguzi, Sheria Zinazosimamia Masuala ya Uchaguzi na matumizi ya TEHAMA katika uchaguzi.

Kikosi Kazi hiyi kimependekeza ushiriki wa wanawake, vijana, watu wenye ulemavu katika siasa, demokrasia na uongozi na utoaji wa elimu ya uraia ikiwemo elimu ya mpiga kura nchini.
Eneo lingine ni kuhusu rushwa na maadili katika siasa na uchaguzi, mfumo wa maridhiano ili kudumisha haki, amani, utulivu na umoja wa kitaifa nchini, mawasiliano kwa umma, vyombo vya habari na siasa na Katiba Mpya ya Tanzania ambapo Kikosi Kazi kinapendekeza kukamilishwa kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya kupitia hatua sita.

“Hatua ya kwanza mjadala wa kitaifa ili kupata muafaka katika masuala ya msingi kabla ya kuanza mchakato wa kuandika katiba mpya.

Mjadala huu ufanyike kwa ushiriki mpana wa wananchi. masuala ya msingi yanajumuisha muundo wa muungano, madaraka ya rais, mfumo wa uchaguzi, madaraka ya serikali za mitaa, rushwa na maadili na mengineyo yatakayojitokeza.

Hatua ya pili: kuhuisha sheria ya mabadiliko ya katiba na sheria ya kura ya maoni, yakiwemo kuainisha muda wa mchakato mzima, kutambua kuanzishwa kwa jopo la wataalam na kuainisha misingi ya kuzingatiwa katika mchakato wa mabadiliko ya katiba.

Aidha, kuwepo na ushirikishwaji mpana wa wananchi katika mchakato wa kuhuisha sheria hiyo, kwa kufuata taratibu za utungaji wa sheria nchini.

Hatua ya nyingine kuundwa kwa jopo la wataalam baada ya sheria ya mabadiliko ya katiba kuhuishwa na mengine mengi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!