Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Makamba akabidhiwa Ofisi, apewa zigo la diplomasia ya uchumi
Habari Mchanganyiko

Makamba akabidhiwa Ofisi, apewa zigo la diplomasia ya uchumi

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amekabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Stergomena Tax katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Waziri Makamba amemshukuru Dk. Tax kwa ushirikiano aliompatia wakati wote tangu yalipofanyika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri mwishoni mwa mwezi Agosti 2023.

“Tangu Mheshimiwa Rais alipofanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri umekuwa ukinipatia ushirikiano wakati wote, nakushukuru sana, pia nakutakia heri katika majukumu yako mapya” amesema Waziri Makamba

Naye Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Tax amesema alipohudumu katika Wizara hiyo alipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa menejimenti na watumishi wa Wizara na kumhakikishia Waziri Makamba kuwa ana watumishi wachapakazi

“Wakati wa utumishi wangu hapa wizarani, nilipata ushirikiano mkubwa, hivyo napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana menejimenti na watumishi wote wa wizara kwa ushirikiano walionipa,” alisema Dk. Tax

Amesema jukumu lililo mbele ya Wizara hiyo ni kutekeleza maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa vitendo kwa kutafuta fursa mbalimbali za kukuza uchumi na kuendeleza diplomasia ya uchumi

Pamoja na mambo mengine, Dk. Tax pia amemtakia utendaji kazi mwema Waziri Makamba na kuwashukuru Naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Mkuu wa Wizara, Balozi Dk. Samwel Shelukindo, Naibu Katibu Mkuu, Menejimenti na watumishi wa Wizara.

Makabidhiano hayo yalihudhuriwa pia na wajumbe wa menejimenti na baadhi ya watumishi wa wizara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!